Habari za Punde

Uzinduzi wa Kamisheni ya Kiswahili Afrika Mashariki Zanzibar.

Jengo la Ofisi za Kamisheni ya Kiswahili Afrika Mashariki Zanzibar limezinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, likiwa katika eneo la maisara.   
 Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Profesa Kenneth Simala akimkaribisha Waziri wa Habari Utamaduni Tanzania Dkt. Harrison Mwakyembe alipowasili katika viwanja vya jengo hilo wakati wa uzinduzi wake.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulizindua jengo la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki Zanzibar.kulia Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt, Augustine P Mahiga.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kulifungua Jengo la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki Zanzibar, kulia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili Afrika Mashariki Profesa Kenneth Simala na kushoto Waziri wa Habari Utamaduni Tanzania Dkt. Harrison Mwakyembe na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud.wakishuhudia uzinduzi huo.Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kamisheni ya Kiswahili Afrika Mashariki Zanzibar. baada ya uzinduzi wa jengo hilo lilioko maeneo ya maisara Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashari wa Kamisheni ya Kiswahili Afrika Mashariki Zanzibar. baada ya uzinduzi wa jengo hilo lilioko maeneo ya maisara Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.