Habari za Punde

Zantel Yatoa Zawadi ya Mbuzi Katika Kusherehekea Sikukuu ya 'Eid Al Hadha ',Yawakumbuka Watoto Yatima na Wazee Zanzibar.

Mwakilishi wa Zantel-Tanga Mansoor Ally, (kulia) akikabidhi mbuzi kwa kituo cha kulea watoto yatima cha Goodwill & Humanity Foundation kilichopo jijini Tanga wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika kituo hicho, siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita ikiwa ni moja ya hatua ya kujitolea kwa jamii kwa Kampuni hiyo. Zaidi ya mbuzi 100 walitolewa katika mikoa mbalimbali ya bara na visiwani katika kuadhimisha sikukuu ya Eid Al Adha.
Meneja wa Data na Vifaa vya Intaneti, Hamza Zuheri (kushoto) akikabidhi mbuzi wawili kwa mwakilishi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Buguruni Swafaa, Zimbwe Hatibu Koja wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi za Zantel jijini Dar es salaam, siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita hii ikiwa ni moja ya hatua ya kujitolea kwa jamii kwa Kampuni hiyo ambapo zaidi ya mbuzi 100 walitolewa katika mikoa mbalimbali ya bara na visiwani katika kuadhimisha sikukuu ya Eid Al Adha. Wengine kwenye picha ni maafisa wa Zantel Emmiliana Vakolawene(kushoto) na Winnes Baldwin Lyaro (wa pili kushoto).
Afisa wa Zantel Abdallah Saadun akikabidhi mbuzi kwa walezi na watoto wa kituo cha kulea watoto yatima cha Mazizini-Zanzibar wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi kuu ya Zantel iliyopo Unguja, siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita ikiwa ni moja ya hatua ya kujitolea kwa jamii kwa Kampuni hiyo ambapo zaidi ya mbuzi 100 walitolewa katika mikoa mbalimbali ya bara na visiwani katika kuadhimisha sikukuu ya Eid Al Adha. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Chapa na Mawasiiano wa Zantel, Rukia Mtingwa.
Afisa Masoko wa Zantel, Deus Mtena (wa pili kushoto) akikabidhi mbuzi kwa Katibu wa kituo cha kulea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Bunju, Bw. Omari Abdu (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi za Zantel jijini Dar es salaam, siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita hii ikiwa ni moja ya hatua ya kujitolea kwa jamii kwa Kampuni hiyo ambapo zaidi ya mbuzi 100 walitolewa katika mikoa mbalimbali ya bara na visiwani katika kuadhimisha sikukuu ya Eid Al Adha. Wengine katika picha ni Afisa Mawasiliano wa Zantel Winnes Baldwin Lyaro (Kushoto) na Mweka Hazina wa kituo cha Mwandaliwa Haji Mahmood Bakhulla.
Afisa wa Zantel Abdallah Saadun akikabidhi mbuzi kwa walezi na watoto wa kituo cha kulea watoto yatima cha Mazizini-Zanzibar wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi kuu ya Zantel iliyopo Unguja, siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita ikiwa ni moja ya hatua ya kujitolea kwa jamii kwa Kampuni hiyo ambapo zaidi ya mbuzi 100 walitolewa katika mikoa mbalimbali ya bara na visiwani katika kuadhimisha sikukuu ya Eid Al Adha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.