Habari za Punde

FUFA Yaomba Kupelekwa Mbele Mashindano ya Beach Soka ya Afrika Mashariki.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Shirikisho la Soka nchini Uganda (FUFA) wameomba kupelekwa mbele Mashindano ya Vilabu Bingwa vya mpira wa Ufukweni ya Afrika Mashariki na kati ambayo yalikuwa yaanze kesho Septemba 5, 2017 Visiwani Zanzibar.

FUFA wameiandikia barua Baraza la vyama vya Michezo Afrika Mashariki CECAFA ambapo wameomba Mashindano hayo yapelekwe mbele kisha yaandaliwe na CECAFA wakishirikiana na Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) ambao ni wenyeji wa Mashindano hayo.

Akizungumza na Mtandao huu Mwenyekiti wa Soka la Ufukweni Visiwani Zanzibar Ali Sharifu "Adolf" amesema Mashindano hayo yalikuwa yaanze Septemba 5, 2017 lakini FUFA wameomba yapelekwe mbele na pia CECAFA waaingie kama ni walezi wa mchezo huo.

"Ni kweli Mashindano yalikuwa yaanze Septemba 5, lakini wenzetu FUFA wamewaomba CECAFA waaingie na wao na pia Mashindano yapelekwe mbele, sasa tunawasubiri CECAFA watatuambia lini yataanza, lakini sisi tumefarijika sana kuona mpaka CECAFA na wao wataingia katika Mashindano hayo ya Vilabu bingwa vya Beach Soka, sasa tunasubiri CECAFA watangaze tarehe ya kuanza". Alisema Adolf.

Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya vilabu 6 kutoka Zanzibar na Uganda ambazo ni Malindi, Green River na Lavister kutoka Zanzibar na kutoka Uganda ni Makerere University, Mutesa 1 Royal University na St. Laurence University.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.