Habari za Punde

Zimamoto yaumiza kichwa kumpata Kocha MpyaNa: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Makamo Bingwa watetezi wa ligi kuu soka ya Zanzibar timu ya Zimamoto ipo katika mchakato wa kutafuta kocha mpya atakaefundisha timu hiyo katika msimu mpya wa mwaka 2017-2018 kwenye ligi kuu soka ya Zanzibar pamoja na Kombe la Shirikisho Barani Afrika.


Katibu wa timu hiyo Ali Ussi Bakar (Jongo) amesema mpaka sasa hawajajua ni mwalimu yupi wamfate ili kuja  kuifundisha timu yao ambayo imepania kufanya vizuri katika msimu huu.


"Tupo katika harakati za kuangalia na kujipanga ili kuona ni mwalimu yupi tutakuwa nae kwenye msimu huu mpya, malengo yetu yapo pale pale kutwaa ubingwa au hata nafasi ya pili kama munavyojua msimu ulopita tulicheza kombe la klabu bingwa Afrika na msimu huu tutacheza kombe la Shirikisho hivyo msimu ujao tena tunataka kucheza tena klabu bingwa ndio mana kwasasa tuna haha kumsaka mwalimu mpya mwenye uwezo wa hali ya juu kama walivyokuwa kina Bares na Seif Bausi". Alisema Jongo.


Kikosi hicho kwasasa kinafundishwa na mwalimu Msaidizi Juma Omar Said baada ya mwalimu alokuwa akiifundisha Seif Bausi kuachana nae.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.