Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Ukimwi (UNAIDS) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ndugu Michel Sidibr
Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi akiagana na waziri wa Oman anayeshughulikia Mafuta na Gesi Dkt Mohammed Bin Hamed. Oman imekubali kuyafanyia ukarabati majengo ya kihistoria ya Beit-Al-Ajab na Palace Museum
Na Mwandishi Wetu OMPR.
Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia ukimwi kwa misaada yake ambayo imesaidia kupunguza maambukizi
ya virusi vya ukimwi nchini.
Makamo wa Pili wa Rais
ameyasema hayo Afisini kwake Vuga wakati wa mazungumza yake na Mkurugenzi
Mtendaji wa Shilika la Umoja wa Mataifa linashughulikia Ukimwi ndugu Michel
Sidibr
Amesema misaada ya Shirika
hilo la UNAIDS imesaidia kuendesha kampeni mbali mbali ambazo zimejenga ualewa
miongoni mwa wananchi kuhusu kuwepo kwa ukimwi nchini.
Hata hivyo balozi Seif
ametoa wito kwa viongozi kuendelea kuwahimiza wananchi kujiepusha na vitendo
vinavyoambukiza ukimwi pamoja na kuwashajihisha kupima mara kwa mara.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
UNAIDS ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema Zanzibar ni
kigezo cha kujivunia kwa nchi nyingi kutokana na mafanikio yake ya kupungunza
kwa kiwango kikubwa maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama mjamzito
kwenda kwa mtoto.
Mkurugenzi Mtendaji huyo
amesema mafanikio ya Zanzibar ya kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi
kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto yakiendelezwa hakutokuwa na mtoto
anayeambukizwa virusi vya ukimwi katika kipindi kifupi kijacho.
Wakati huo huo Makamo wa
Pili wa Rais Balozi Seif amekuwa na mazungumzo na Waziri wa Oman
anayeshughulikia Mafuta na Gesi Dkt. Mohammed bin Hamed.
Katika mazungumzo yao
Balozi Seif ametoa shukrani zake kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kwa Oman kwa misaada yake katika miradi mbali mbali ya maendeleo.
Balozi Seif ameiomba Oman
kusaidia katika upanuzi wa uwanja wa ndege wa Pemba na kuwa wa kimataifa, ombi
ambalo Serikali ya Oman imesema italifikiria.
Balozi Seif amesema uwanja
huo utasaidia kukuza biashara ya utalii na viungo kati ya nchi hizo mbili
pamoja na kuwauganisha kwa karibu zaidi watu wa Zanzibar na Oman ambao kwa
asili ni ndugu.
Kwa upande wake Waziri huyo
wa Mafuta na Gesi Dkt Mohammed bin Hamed safari yao ya meli kuja kwa ndugu zao
wa Zanzibar kuna lengo la kufungua ukurasa mpya wa mashirikiano kati ya pande
hizo mbili.
Amesema kuna mambo mengi ya
kuwaunganisha watu wa pande hizo mbili kuliko mambo ya kuwatenganisha.
Kuhusu ombi la Zanzibar la
kukarabati kumbusho la Beit-al-ajab na kumbusho la Palace, Serikali ya Oman
imesema iko tayari kuyafanyia matengenezo makubwa majengo hayo kwani ni
rasilimali ya ulimwengu mzima.
No comments:
Post a Comment