Habari za Punde

Kampuni ya Bima ya Resolution Yazindua Njia ya IRAP Ili Kuwajengea Uwezo Wafanyakazi Wake Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya Resolution Bw. Peter Nduati akielezea mabadiliko mbalimbali ya kampuni,katika utendaji kazi na kuwajibika kwa wafanyakazi na kuwasisitiza kuchapa kazi zaidi.


Wafanyakazi wa Resolution Insurance wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu Bw. Peter Nduati wakati akiongea nao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya  Resolution  Tanzania Bi. Maryanne Mugo akieleza kwa ufupi kuhusu IRAP na changamoto zake.
Meneja wa Rasilimali Watu na Rasilimali Bi. Jennifer Mburu (kushoto) wa Kampuni ya Bima ya Resolution  akielezea Maana kamili ya IRAP na jinsi wafanyakazi wa Resolution watakavyotakiwa kuishi na Filosofia hiyo ili Kuboresha utendaji pamoja na Kumhudumia mteja kwa weredi. Kulia ni Bw. Melchizedek Muro Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja kutoka Resolution.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Dharura kwa Wateja kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution Bi. Batuli Karya akitoa mrejesho baada ya Chemsha Bongo kwa wafanyakazi kumalizika.
Bi. Petronella Mwasanduba ambaye ni Mwenyekiti wa Rasilimali watu wa Kampuni ya Bima ya Resolution-Tanzania akitoa majumuisho baada ya wakurugenzi kueleza jinsi ya utendaji mpya wa kazi wenye tija.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Resolution wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Dharura kwa Wateja Bi. Batuli Karya(hayupo Pichani) wakati wa mrejesho wa Chemsha Bongo
Bw. Alphonse Michael (wa kwanza kulia) ambaye ni Mshauri Mkuu wa Biashara kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution Tanzania akitoa mwongozo wakati wa uzinduzi wa IRAP kwa ajili ya kuwajengea uwezo wafanyakazi.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya Resolution wakiwa katika  Chemsha Bongo 
Mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Bima la Resolution Bw. Melchizedek Nyau akisoma swali wakati wa zoezi la chemsha bongo ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo wafanyakazi
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya Resolution wakirusha  Njiwa juu ishara ya uzinduzi rasmi wa IRAP
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya Resolution Bw. Peter Nduati akizindua Michezo kwa ajili ya kujengea uwezo wakafanyakazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution Tanzania Bi. Maryjanne Mugo akizindua Michezo kwa ajili ya kujengea uwezo wakafanyakazi.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya Resolution wakiwa wanaendelea na michezo mbalimbali
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya Resolution Bw. Peter Nduati (kushoto) akitoa zawadi kwa wafanyakazi.
Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.