Habari za Punde

Ligi Daraja la Kwanza Taifa Pemba Timu Umeme Yaimulika Cossovo.

Na. Haji Nassor - Pemba.

KIRINDANDA cha ligi daraja la kwanza taifa Pemba, kimeendelea tena kuchanjanja mbuga, kwenye viwanja tofauti, ambapo kwenye nyasi za Gombani, timu ya Cossovo ya Wambaa, imejikuta ikichomwa kwa bao 1-0 na timu ya Umeme, mchezo uliopigwa majira ya saa 10:00 jioni.

Mchezo huo uliohudhuriwa na watazamaji wachache, ulianza kwa timu hizo kusoma mchezo, ambapo washambuliaji na walinzi, walikuwa wakipeana pasi fupi fupi, ili kutamfuta namna ya kujipatia bao.

Dakika ya 35, Cossovo walifanya shambulio zito langoni mwa Umeme, baada ya mpira ulioanzia kwa mlinda mlango wao, na kutua katikati ya dimba, ingawa washambuliaji wao, walimalizia kwa pasi butu na mpira kutoka nje.

Dakika ya 37, Umeme ilijipatia bao pekee lililofungwa na mwanandinga wao Mohamed Haji, baada ya kuwaramba chenga walinzi wawili wa Cossovo, kisha kujaribu kombora lililojaa wavuni kwa ufundi.

Dakika 90 zikamalizika, kwa Cossovo kuondola patupu, huku Umeme ikijitengezea mazingira mazuri, kwenye michuano hiyo ya lidi daraja la kwanza taifa Pemba.

Na katika mchezo mwengine uliosukumwa uwanja wa FFU Finya, wenyeji wa uwanja huo, timu ya Selem view waliutumia vyema uwenyeji wao, kwa kuichapa Machomane bao 1-0 likifungwa na Mohamed Saad dakika 59.

Ligi daraja la kwanza taifa Pemba, baada ya kuwa mapunziko jana, itaendelea tena leo kwenye uwanja wa FFU Finywa kwa Juhudi Pembeni, kuwaalika Mila ya Kangani, ambapo kesho ni zamu ya Manta na Umeme Gombani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.