Habari za Punde

Ligi kuu Zanzibar Kituo Cha Pemba, Kuendelea leo Katika Viwanja vya Gombani na FFU Finya.

Na.Haji Nassor - Pemba.

LIGI kuu ya Zanzibar kituo cha Pemba, baada ya kuwa kwenye likizo fupi, itarudi tena leo, kwa viwanja viwili vya Gombani na FFU Finya, kuwa mashakani, kwa miamba minne kuonyesha ufundi wa kusakata soka.

Kwenye uwanja wa Gombani, kutakuwa na sege nnega ya aina yake, kwa timu ya Chuo basra yenye point mbili kwa michezo miwili, wakiwa wageni wa Younge Islanders ambayo ina alama tatu, wakiwa sawa kwa idadi ya michezo.

Islanders inatupa karata yake tena, baada ya mchezo wa awali kushinda kwa bao 1-0, ambapo mchezo wa pili wakafungwa bao kama hilo na FSC.

Leo pia kwenye uwanja wa unaomilikiwa na FFU, mitaa ya Finya Okapi yenye alama moja, watakuwa wenyeji wa dimba hilo, na watawatandikia jamvi wageni wao timu ya Hard Rock, ambayo ina point mbili kibindoni.

Kesho kutakuwa na mchezo mmoja tu, ndani ya dimba la Gomani mjini Chakechake, kwa wanagenzi wa ligi ya Zanzibar timu za Dogo moro yenye point moja, ikikwaruzana na Wawi star, ambayo hajanusa point hata moja, licha ya kushuka uwanja mara mbili.

Wakati ligi kuu ya Zanzibar kituo cha Pemba, ikiendelea tena leo, kiti cha usukani kinaendelea kukaliwa na timuza Mwenge na FSC zenye point sita kila mmoja, huku News star ikiwa ya  tatu kwa kwa point zake nne, wakati timu zenye point tatu tatu ni Chipikizi, Shaba, Islanders na Kizimbani. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.