Habari za Punde

Mashabiki wa Timu ya Simba na Yanga Zanzibar Wajumuika Pamoja kutizama Pambano Hilo Kupitia TV Kwa Kiingilio cha Shilingi Elfu Moja.Katika Maskani yao Amaan Unguja Timu Hizo Zimetoka Sare ya Bao.1 - 1. Kastika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Wapenzi wa Timu za Yanga na Simba Zanzibar wakiwa katika maskani ya ya Amaan maarufu kwa jina la Amaan miligotini wakiwa pamoja kuangalia Mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchezo uliofanyika leo jioni katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Timu hizo zimetoka Sare ya bao 1 -1. Wapenzi hao wamejumuika pamoja kwa kulipia kiingilio cha shilini 1000/- ili kuweza kuoona mpira huo kupitia kingamuzi cha Azam Tv, Hawa wote wamelipia kiingilio ili kuchangia Timu zao.
Viongozi wa Maskani za Timu za Yanga na Simba katika eneo la Amaan Zanzibar wakikatisha tiketi kwa wanachama wao ili kuweza kuona pambano la Watani wa Jadi Simba na Yanga kupitia luninga katika kingamuzi cha Azam TV.
Viongozi wa Maskani za Timu za Yanga na Simba katika eneo la Amaan Zanzibar wakikatisha tiketi kwa wanachama wao ili kuweza kuona pambano la Watani wa Jadi Simba na Yanga kupitia luninga katika kingamuzi cha Azam TV.
Wapenzi wa Simba na Yanga wakifuatilia mpambano huo kupitia luninga Zanzibar.

Wapenzi wa Simba wakishangilia bao la Timu yao lililofungwa na Kichuya katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

Wapenzi wa Timu ya Yanga wakishangilia bao la timu yao la kusawazisha lililofungwa na mshambuliaji wa Yanga Chirwa katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.