Habari za Punde

Mradi wa Champion Heath Wanufaisha Vijana 98 wa Unguja na Pemba Unaosimamiwa na Milele Zanzibar Foundation.

Mratibu Miradi ya Elimu Shirika la Milele Zanzibar Foundation Ali Bakari Omar akizungumxza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Vijana wanaopata Elimu ya Chuo Kikuu kupitia Mradi wa Champion Heath ukiwa chini Shitrika la Milele Zanzibar Foundation, Vijana 98 wamepata ufadhi wa kusomea masomo ya Afya ili kusaidia Jamii Vijijini Unguja na Pemba, Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezio wa kuibuwa miradi wanapomaliza masomo yao ya Chuo cha Afya Mbweni.
Baadhi ya Vijana 98 wa Champion Heath wanaopata ufadhili ya masomo ya Afya wakiwa katika mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wa kuibua miradi yanayofanyika katika ukumbi wa Chuo cha SUZA majestik Zanzibar. 
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dr. Fadhil Mohammed akitowa nasaha zake wakati akifungua mafunzo ya Siku Tatu kwa Vijana wa Mradi wa Champion Heath unaosimamiwa na Milele Zanzibar Foundation, mafunzo hayo yanafanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha SUZA majestik Zanzibar na kuwashiriki Vijana hao kutoka Unguja na Pemba wanaosomea masomo ya Afya kwa Jamii.kulia Mkufunzi wa Mafunzo hayo kutaka Tanzania Bara Edson Nyingi na kushoto Mratibu wa Miradi ya Elimu Milele Zanzibar Foundation Ali  Bakari Omar.   
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dr. Fadhil Mohammed, akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo hayo kwa Vijana 98 wanaofadhiliwa na Milele Zanzibar Foundation kupitia Mradi wake wa Champion Heath, ili kutowa huduma ya Afya kwa Jamii ya Vijini Unguja na Pemba. 
Washiriki wa Mradi wa Champion Heath wakifuatilia ufunguzi huo wa mafunzo yao ya Siku Tatu ya kuwajengea uwezo wa kuibua miradi unaotolewa kwao baada ya kumaliza masomo yao ya Afya kupitia ufadhili ya Milele Zanzibar Foundation.
Mkufunzi wa mafunzo hayo Edson Nyingi akitowa Mada wakati wa mafunzo hayo ya siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha SUZA majestik Zanzibar No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.