STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 30.10.2017

RAIS wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amemtumia
salamu za pongezi Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan kwa
kutimiza miaka 94 tokea kuanzishwa kwa Jamhuri ya Uturuki.
Katika salamu hizo Dk. Shein alieleza kuwa
wananchi wa Zanzibar wanaungana pamoja na ndugu zao wa Uturuki katika
kusherehekea siku hii adhimu na muhimu katika historia ya nchi hiyo.
Aidha, salamu hizo, zilieleza kuwa tukio hilo
kubwa, linatoa nafasi ya kuendeleza uhusiano na ushirikiano mkubwa kati ya Jamhuri
ya Watu wa Uturuki na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alimtakia kiongozi
huyo pamoja na familia yake na wananchi wote wa Jamhuri ya Uturuki afya na sherehe
njema katika kuadhimisha siku hiyo huku akimtakia kiongozi huyo mafanikio zaidi
katika kuendelea kuipatia maendeleo zaidi ya kiuchumi nchi hiyo kwa madhumuni
ya kulinufaisha Taifa hilo pamoja na watu wake.
Jamhuri ya Uturuki ilianzishwa mwaka 1923 na
Jenerali Kemal Ataturk ambayo iliundwa na kuwa Taifa baada ya vita vikuu vya
Kwanza vya dunia ambapo kabla ya hapo Waturuki walikuwa chini ya milki ya Osmani
(Ottoman Empare) iliyounganisha mataifa mengi ya Sultan wa Konstantinopoli
wakati huo.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment