Habari za Punde

Simba wamaliza kambi Zanzibar na kurejea Dar

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kikosi cha Simba kimeondoka Visiwani Zanzibar leo saa 3 za asubuhi kwa Ndege na kurejea jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mwisho ya mechi yao ya kesho ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na Mtandao huu wakati waondoka hapa Zanzibar kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema akili yao yote ni kuifunga Yanga kesho kwenye uwanja wa Uhuru huku akiwataka Mashabiki wa Simba waendelee kuishangiria timu yao.

“Kambi ya Zanzibar ilikuwa nzuri sana naamini tumefikia malengo yetu, hapa tunaondoka na leo jioni Dar tutafanya mazoezi ya mwisho, nawaomba Mashabiki wa Simba wazidi kuishangiria timu yao”. Alisema Manara.

Simba walikuwa kambini mjini hapa tangu Jumatatu ya Oktoba 23 na leo Ijumaa Oktoba 27 wamerejea nyumbani Dar es salam kuwavaa Yanga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.