Habari za Punde

King akiri hali ya Miembeni City ni ngumu, ahakikisha kutoshuka daraja

Kocha wa Miembeni City, Mohammed Seif "King"Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kocha Mkuu wa timu ya Miembeni City Mohammed Seif "King" amekiri hali ya klabu yake si nzuri kufuatia kucheza michezo saba mfululizo bila ya kupata ushindi hata mchezo mmoja katika ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja.

King amesema kwa mara ya kwanza anakumbana na matokeo mabaya katika maisha yake ya soka lakini bado hajakata tamaa kwenye ligi hiyo huku akiamini vijana wake watapambana kufa na kupona ili wabakie kwenye ligi Kuu.

"Balaa balaa, katika historia yangu kwa mara ya kwanza nakumbana na matokeo mabovu kama haya, nakiri tuna matatizo lakini tutapigana kufa kupona ili tubakie kwenye ligi, na kushuka daraja pia sio dhambi lakini vijana watahakikisha tunabakia". Alisema King.

Miembeni City ipo nafasi ya 13 wakiwa na alama 1 tu kwenye ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja kufuatia kufungwa michezo 6 na kwenda sare mchezo mmoja ambapo mpaka sasa City wapo kwenye mstari mwekundu kwenye ligi hiyo yenye jumla ya timu 14 ambapo timu 6 za chini zitalazimika kushuka daraja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.