Habari za Punde

Kivazi cha stara, heshima kiwavae waandishi wa habari


NA HAJI NASSOR, PEMBA
TASNIA ya habari, ni muhimili wa nne usiotambulika rasmi hadi sasa, kwenye maandishi na vitabu vya mataifa mbali mbali, ingawa kutokana na utendaji wao wa kazi, unaelekea kuwa muhimili kamili.
Waandishi wa habari wamekuwa wakitajwa, kukosoa, kuelimisha, kuhabarisha na hata kuhoji muhimili mwengine, kwa maana ya kuwa katikati baina ya mihimili mitatu ya dola.
Waandishi wa habari wenyewe, wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha jamii ilioizunguruka, inaipasha habari na matukio mbali mbali, ambapo hilo ni haki ya kikatiba.
Lakini kinachonilete mbele yenu leo hii  ni kuwataka waandishi hao wa habari kuhakikisha kivazi wanachovaa kiwe cha heshima na stara kwao.
Maana wapo waandishi wa habari aidha wawe wanawake au wanaume, wamekuwa na kivazi chenye kuleta mashaka sio tu waandishi wenzao, lakini hata jamii wanayoihudumia.
Jamii imekuwa ikiwacha midomo wazi pale wanapomuona mwandishi wa habari anaetarajiwa kuwa muhimili wa nne wa dola, lakini kivazi chake hakifai hata kulala nacho.
Wapo waandishi hao, wamekuwa wakivaa nguo nyingi na pengine za gharama kuwab, lakini ilioko ndani, basi unaweza kuiona tena hata kwenye uoni hafifu.
Na wakati mwengine mwandishi huyo wa habari, anakwenda kuzungumza na jamii, ilioko vijijini au hata watu wenye vyeo, lakini hujitoa mshipa wa fahamu, kwa kwenda uchi kwa lugha fupi.
Wapo wanaojiuliza kwa baadhi ya waandishi wa habari kutovaa kivazi chenye heshima na kujistiri, ndio uandishi wa habari, ndio unaweza kupata habari iliojificha, au ni kukiuka maadili ya dini?
Maanana inapotokezea waandishi hao wamefuatana na wengine waliojistiri, huwa kama mchunga aliefuatana na mnyama wake, huku yeye akiwa amejistiri lakini mnyama wake hana nguo.
Ivyo ni chombo gani ndani ya taifa, au watua gani watakaoona kuna umuhimu wa mrengo wa kihabari uwe kama muhimili wa nne wa dola, kwa hali ilivyo kwa waandishi hao wa habari hasa kwa upande wa kivazi?
Leo sitaki nigusue suala la elimu, maana linasehemu yake siku nyengine, lakini basi hata kuvaa nguo ya stara linamsubiri kiongozi wa nchi aseme au kutungwe sheria maalum?
Kila mmoja anahudhuria kwenye nyumba ya ibada kwa mujibu wa imani yake, sasa chakujiuliza iko dini au imani fulani inayoruhusu mtu kwenda nusu uchi?
Kama haipo iweje hawa baadhi ya wanahabari tena wengine wabobevu wa taaluma hiyo, lakini ni aibu, fedheha na haingii akili kivazi wanachovaa.
Mimi sitii mguu leo kwa wale wanaojipamba mpaka kupita kiasi la hasha, pengine kama wamejistiri, basi darsa lao la kuwataka kupunguza mapambo litakuwa siku nyengine.
Kama hivyo ndivyo, lazima waandishi hao wa habari wajiangalie upya juu ya kivazi chao wanacho vaa iwapo dini wanayoifuata inaruhusu, maana pengine kwa kuambiwa kwa mdomo bado ni wa sugu.
Lakini hata nyinyi waandishi wa habari, sio mnazo Jumuia zenu, basi zitumieni pia kwa kukumbushana juu ya aina ya kivazi chenye stara kwa baadhi hao waandishi, ili wasiwatie doa na wengine.
Na Wizara inayoowagoza waandishi hawa wa habari, kwa vile ipo tena macho haijalala, mnapokutana na waandishi hawa wa habari, hebu wakumbusheni na jukumu lao la kutunza utamduni wa kivazi cha asili tena cha kujistiri.
Lakini hata wazazi, walezi, waume au hata wake wa waandishi wa habari wasiopenda kuvaa kivazi cha stara na chenye heshima, lazima muwe wakali kwa hili.

Naamini kila kitu kinawezekana, iwapo kila mmoja atatekeleza wajibu wake bila ya kusimamiwa na kukakikisha anaheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.