Habari za Punde

Kukosekana kwa nishati ya Jua kunavyoathiri ukaukaji wa karafuu

 SHUNGU ya karafuu mbichi za mkulima Mohamed Issa Salum, aliepiga kambi kijiji cha Gongoni shehia ya Kipapo wilaya ya Chakechake Pemba, zikianza kuharibika kutokana na kukosa jua, ambalo ndio nishati pekee hadi sasa, inayotumika kwa ajili ya kukaushia karafuu hizo, ili zibakie kwenye kiwango chake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WAZIRI wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa rais Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed, akizingalia karafuu za mkulima Mohamed Issa, wa Gongoni Kipapo wilaya ya Chakechake, ambapo juzi wakati anamtembelea, alililia kuharibika kwa karafuu zake, kutoka na kukosekana kwa nishati ya jua, Waziri huyo alikuwa na ziara kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MCHUMAJI wa karafuu (kibarua) ambae hakupatikana jina lake, akiendelea kuliokoa zao la karafuu, kwenye shamba la mkulima Mohamed Issa, alieweka kambi kijiji cha Gongoni, shehia ya Kipapo wilaya ya Chakechake, ambapo kwa sasa wachumaji (vibarua), wanalipwa kati ya shilingi 2,000 hadi shilingi 2,500 kwa pishi moja, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WAZIRI wa nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed, akiungana na watendaji mbali mbali wa ofisi yake, ZSTC na wizara ya Kilimo wakichuma karafuu kama kutia baraka, kwenye shamba la mkulima Mohamed Issa Salum wa Kipapo wilaya ya Chakechake, wakati Waziri huyo na ujumbe ulipomtembelea mkulima huyo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).     

MDHAMINI ZSTC Pemba, Abdalla Ali Ussi, akiziangalia karafuu za mkulima Mohamed Issa Salum, kutokana na kukosa jua, kwenye ziara ya Waziri wa nchi afisi ya makamu wa pili wa rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed, ambae aliwatembelea wakulima kadhaa wa karafuu, hivi kraibuni kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.