Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani 2017, Wananchi wapewa Tahadhari

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Leonard Subi (kushoto) akifanya uchunguzi wa afya yake kwenye maadhimisho hayo ya Siku ya Kisukari Duniani 2017 yaliyofanyika kwa mkoa wa Mwanza katika uwanja wa Nyamagana jana.
 Dkt.Subi akifanya uchunguzi wa macho kwa kutazama namba maalumu mebele yake.
 Mtaalamu wa afya akionyesha namba maalumu zinazotumika kufanyia utambuzi wa uono.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonard Subi akipokea maelezo kutoka banda la Abacus Pharma ambao ni wauzaji wa bidhaa za Sugar Free zisizo na athari ya kumsababishia mtumiaji ugonjwa wa kisukari.
Mwakilishi wa kampuni ya Abacus Pharma, Jeremiah Bwana (katikati), akitoa maelezo kwa Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonard Subi kuhusiana na bidhaa za Sugar Free

Na Binagi Media Group
Novemba 14 kila mwaka Tanzania huungana na mataifa mbalimbali kuadhimisha Siku ya Kisukari Duniani ambapo pamoja na mambo mengine, lengo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa kisukari ili kutambua namna ya kujiepusha na ugonjwa huo.

Katika kuadhimisha maadhimisho hayo mwaka huu yaliyofanyika jana, Chama cha Watoa Huduma za Afya Tanzania APHTA kwa kushirikiana na hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure, kilitoa fursa kwa wananchi kupima afya zao bure kwa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari.

Maadhimisho hayo kwa mkoa wa Mwanza yalifanyika kwenye uwanja wa Nyamagana ambapo mgeni rasmi ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Leonard Subi anawahimiza wananchi kuzingatia ulaji sahihi wa vyakula pamoja na kufanya mazoezi ili kujiepusha na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo kisukari.

Hata hivyo wananchi wanahimizwa kupima afya zao mara kwa mara ili kuepuka madhara wanayoweza kukumbana nayo kutokana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari, ikizingatiwa kwamba watanzania tisa kati ya 100 wenye umri wa miaka 25 na kuendelea wana ugonjwa wa kisukari ambapo kati ya hao tisa, ni wagonjwa wawili tu wenye kutambua kwamba wanaugua ugonjwa huo.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.