Habari za Punde

Mashindano ya Chalenji Yasogezwa Mbele Zanzibar Heroes yazidi kupikika

                                                   .
Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limesogeza mbele Mashindano ya Kombe la Chalenji.
Mashindano hayo yalitarajiwa kuanza Novemba 25 hadi Disemba 9, 2017 lakini sasa yataanza Disemba 3 hadi 17, 2017 nchini Kenya.

Akizungumza na Mtandao huu Afisa Habari wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Ali Bakar "Cheupe" ametoa taarifa kuhusu kupelekwa mbele Mashindano hayo.

"Tumepokea Barua kutoka CECAFA kuwa mashindano ya Chalenj yamesogezwa mbele mpaka Disemba 3 kwaiyo timu yetu itaendelea na mazoezi kujiandaa na mashindano hayo". Alisema Cheupe.

Jumla ya Mataifa 12 yanatarajiwa kushiriki Mashindano hayo wakiwemo wenyeji Kenya, Uganda, Somalia, Sudan, Ethiopia, Sudan ya Kusini, Burundi, Rwanda, Tanzania bara, Zanzibar, huku Libya na Zimbabwe zikialikwa kuchukua nafasi ya Djibouti na Eritrea.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.