Habari za Punde

Wachezaji 24 Zanzibar Heroes watajwa waondoka leo kuelekea Nairobi

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes)  itaondoka nchini leo kuelekea Nairobi, Kenya kwa basi tayari kushiriki mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba 3-17, 2017.

Jumla ya msafara wa watu 34 wakiwemo viongozi pamoja na wachezaji 24 wataondoka saa 6 za mchana kwa Boti kisha wakifika Dar es salam watapanda Basi kwenda mpaka Mkoani Tanga watalazimika kulala hapo, kisha asubuhi yake kuanza safari nyengine mpaka Mombasa na wakifika Mombasa watapanda Treni mpaka Nairobi.

Wachezaji 24 waliochaguliwa kuwakilisha kikosi hicho ni :-

WALINDA MLANGO
Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe), Nassor Mrisho (Okapi) na Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU).

WALINZI 
Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahim Mohammed "Sangula" (Jang'ombe Boys), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Issa Haidar "Mwalala" (JKU), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).

VIUNGO 
Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe),Mudathir Yahya (Singida United), Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman "Pwina" (JKU) na Hamad Mshamata (Chuoni).

WASHAMBULIAJI 
Suleiman Kassim "Seleembe" (Majimaji), Kassim Suleiman (Prisons),  Feisal Salum (JKU),  Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri), Seif Abdallah “Karihe” (Lipuli) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).

Awali wachezaji hao walikuwa 30 na kulazimika kuachwa 6 ambao wengine waliachwa kwasababu ya majeruhi akiwemo Matteo Anton (Yanga), Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe), Salum Songoro (KVZ) na Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege) huku wengine walioachwa ni Mbarouk Marshed (Super Falcon) na Omar Juma "Zimbwe" (Chipukizi).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.