Habari za Punde

Zanzibar kufanyika Special Olympic kwa mara ya kwanza



 Makamo Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Mashindano, Mohd Mwinyi Ramadhan

Kamati tendaji ya olimpiki maalum ya wartu wenye ulemavu

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mashindano ya Olimpiki Maalum yanatarajiwa kufanyika Disemba 8 mwaka huu ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika Zanzibar katika Uwanja wa Amaan.

Michezo hiyo ambayo inashirikisha  watu wenye ulemavu wa akili Tanzania nzima na mwaka huu zaidi ya wanamichezo 600 kutoka mikoa mbali mabli kushindana kwenye mchezo wa soka, mpira wa Wavu pamoja na Riadha.

Akizungumzia matayarisho kuelekea Mashindano hayo Mohd Mwinyi Ramadhan ambae ni Makamo Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo amesema leo wamekutana na viongozi kutoka Tanzania bara ili kuzidi kupanga maandalizi ya Mashindano hayo.

“Tumekutana na wenzetu kutoka Tanzania bara kwaajili ya kupanga Mashindano yetu haya, tumefarijika sana kufanyika hapa kwetu mashindano haya na mpaka sasa maandalizi yanaendelea vizuri naamini kila kitu kitakwenda kama tulivyopanga”.

Nae Chalse Res ambae ni mtendaji mkuu wa Olimpik Maalum amewataka Wazazi, kampuni na mashirika mengine yenye uwezo wa kusaidia kufanikisha mashindano haya wajitokeze kuwasaidia Special Olympics, ili kuwaunga mkono katika harakati zao za kuhakikisha walemavu wa akili wanapata haki ya kucheza na kufurahi.

“Mimi nawaomba wananchi wachangie chochote ili vijana wetu na wao wajisikie katika jamii, michezo gharama tunategemea pia msaada wa Watanzania”.

Special Olympics kwa wale wasiofahamu ni programu ya kimataifa ya michezo, kwa watu wenye ulemavu wa akili na ilianzishwa kwa lengo la kuwapa fursa watu hao kujifunza stadi za maisha na kukubalika katika jamii kupitia michezo ambapo lengo ni kupata wachezaji wa kwenda kushiriki michuano ya dunia nchini Abu Dhabi mwaka 2019.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.