Habari za Punde

Baraza la Mji Chakechake latoa msaada wa mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa skuli ya Furaha

 BANDA  la Vyumba vine vya Kusomeshea wanafunzi na stoo moja, la skuli ya Msingi Furahaa Wilaya ya Chake Chake, likiwa katika harakati za ujenzi baada ya baraza la Mji Chakechek kuchangia matufali 3500 na mifuko 100 ya saruji.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
 MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid (Kushoto), akimkabidhi matufali 3500 Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi wa Skuli ya Msingi Furaha Yahya Said Seif, makabidhiano hayo pia yalishuhudiwa na Mkurugenzi wa Baraza la Mji huo Nassor Suleiman Zaharan mwenye koti.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
 MIFUKO 100 ya Saruji iliyotolewa na baraza la mji chake chake, kwa ajili ya ujenzi wa mabanda manne na stoo katika skuli ya Furaha Msingi, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na baraza hilo kusaidia jamii.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid (Kushoto), akimkabidhi mifuko 100 ya saruji Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi wa Skuli ya Msingi Furaha Yahya Said Seif, makabidhiano hayo pia yalishuhudiwa na Mkurugenzi wa Baraza la Mji huo Nassor Suleiman Zaharan mwenye koti.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.