Habari za Punde

Siri ya Zanzibar Heroes kufanya vizuri yatajwa: Ni Umoja wetuKiungo wa Zanzibar Heroes, Abdul Aziz Makame ambae aliifungia Zanzibar Heroes goli la kwanza dhidi ya Uganda Cranes na kuchaguliwa nyota wa mchezo Man of the match.


Na Abubakar Khatib Kisandu, Machakos Kenya.

Kiungo wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Abdul aziz Makame (Abui) ameweka hadharani siri kubwa iliyowapelekea kufanya vyema katika Mashindano ya Cecafa  Senior Challenge Cup yanayoendelea nchini Kenya.

Makame amesema umoja wao ndio silaha kubwa kwao mpaka wakafanikiwa kutinga fainali katika Mashindano hayo.

“Sisi tunapendana sana, yani tuna umoja wa hali ya juu sote wachezaji, viongozi mpaka Mashabiki wetu, tunapokosea tunafahamishana kwa lengo la kutengeneza si kubomoa ndio maana sasa tumefika fainali”. Alisema Makame.

Makame alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo (Man of the Match) katika mchezo wa nusu fainali ya pili kati ya Zanzibar na Uganda ambapo Zanzibar ilishinda 2-1 na kesho Jumapili saa 9:00 Alaasiri Zanzibar itacheza fainali na wenyeji Kenya mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.