Habari za Punde

Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora
Droo ya Hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya maarufu kwa jina la Champions League imepangwa na kuna michezo mitatu ambayo imeonekana kuwavutia watu wengi.


Juventus wanatarajia kukutana na Tottenham Hotspur wakati ambapo wababe wa Hispania Real Madrid wao watakula sahani moja na wababe wa Ufaransa, Paris Saint-Germain.

Ratiba hiyo inamaanisha kuwa staa wa PSG, Neyamr atakutana na Real Madrid kwa mara nyingine baada ya mchezaji huyo kukuna nao mara kadhaa lipokuwac akiitumikia Barcelona.

Gumzo zito ni juu ya  Chelsea wanaonolewa Kocha Antonio Conte ambapo wanatarajiwa kukutana na Barcelona.

Manchester City wao wataanzia ugenini ambapo huko watakipiga dhidi ya Basle wakati Porto wataikaribisha timu nyingine ya England, Liverpool katika hatua hiyo.

Sevilla wao wataanza nyumban I kuikaribisha Manchester United kabla ya timu hizo kurudiana wiki moja baadaye.

Michezo ya hatua hiyo itachezwa Februari, mwakani.

Ratiba kamili ya hatua hiyo ni hii hapa:
Juventus vs Tottenham Hotspur

Basle vs Manchester City

Porto vs Liverpool

Sevilla vs Manchester United

Real Madrid vs Paris Saint-Germain

Shakhtar Donetsk vs Roma

Chelsea vs Barcelona

Bayern Munich vs Besiktas

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.