Habari za Punde

Mahakama Yaamuru Kumrudisha Rumande Aliyekuwa Mwenyekiti UVCCM Taifa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imeamuru kurudishwa tena rumande hadi December 19, 2017 aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM na Mbunge wa Donge, Zanzibar Sadifa Juma Khamis.

Mwenyekiti huyu anadaiwa kukamatwa nyumbani kwake Dodoma December 9, 2017 kwa madai kwamba alikamatwa akiwapa wajumbe soda kutoka Kagera na kosa la pili aliwaahidi kuwalipia nauli.

Sadifa alifikishwa Mahakamani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma 

Sadifa ambaye pia ni mbunge wa Donge, Zanzibar amefikishwa leo Jumatatu Desemba 11,2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma kwa makosa mawili.

Kamanda wa Takukuru mkoani Dodoma, Emma Kuhanga alisema jana Jumapili Desemba 10,2017 kuwa Sadifa angefikishwa mahakamani leo.

Alisema kiongozi huyo alikamatwa nyumbani kwake akituhumiwa kwa kuwapa soda wajumbe wa UVCCM kutoka Mkoa wa Kagera kitendo ambacho ni kinyume cha maadili.

Kuhanga akithibitisha kukamatwa kwa Sadifa alisema alikamatwa Jumamosi Desemba 9,2017.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.