Habari za Punde

Mazishi ya askari wa JWTZ kisiwani Pemba

VIONGOZI mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, vikosi vya Ulinzi na Usalama Kisiwani Pemba, wakiongozwa na wakuu wa mikoa miliwi ya Pemba, wakisubiri kuupokea mwili wa Mraehemu MT 94601 PTE Hamad Haji Bakari, liyefariki dunia nchini DRC CONGO wakati akiwa katika ulinzi wa Amani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
ASKARI wa JWTZ Kisiwani Pemba, wakiwa na huzuni na kusubiri kuupokea mwili wa marehemu MT 94601 PTE Hamad Haji Bakari, katika uwanja wa ndege wa Pemba kwa ajili ya kwenda kuupeleka katika malazi yake ya milele Gombeume Wilaya ya Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WAZIRI asiye na Wizara maalumu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe:Said Soud Said akiteremka katika ndege maalumu iliyobeba mwili wa marehemu MT94601 PTE  Hamad Haji Bakari, aliyefariki dunia wakati akiwa katika shuhuli za kulinda amani nchini DRC CONGO.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla akisalimiana na Waziri asiye na Wizara maalumu Zanzibar, Mhe:Said Soud Said wakati alipowasili kwa ajili ya kushiriki mazishi ya Marehemu MT94601 PTE Hamad Haji Bakari.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
ASAKARI wa gwaride wa JWTZ wakiwa wameubeba Mwili wa Marehemu MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, aliyefariki dunia akiwa katika shuhuli za ulinzi wa Amani nchini DRC CONGO na kuzikwa kijijini kwao Gombeume Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Kisiwani pemba, wakitoa heshima zao baaya ya mwili wa marehemu MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, ulipowasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba, kwa lengo la kupelekwa kijijini kwao kwa mazishi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WAZIRI Asiye na Wizara Maalumu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe:Said Soud Said katikati, akiwa na viongozi mbali mbali wa Serikali, Makamanda wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Pemba, wakitoa heshima zao za mwisho katika kuuwaga Mwili wa Marehemu MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, wakati wmili wake ulipofikishwa kijijini kwao Gombeume Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa mazishi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
ASKARI mbali mbali wa JWTZ Kisiwani Pemba, wakiwa na huzuni baada ya kuwasili kwa mwili wa askari mwenzao, MT94601 PTE Hamad Haji Bakari alipowasili kijijini kwao kwa mazishi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
VIJANA na Watoto mbali mbali wakiangalia mwili wa marehemu kaka yao MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, wakati ulipokuwa ukiangwa katika kijijini kwao Gombeume Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othaman, akitoa salamu za wananchi wa Pemba, kwa familia na wafanyakazi wenzake Marehemu MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, wakati mwili wake ulipofikishwa kijijini kwao kwa ajili ya kuzikwa.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WAZIRI asiye na Wizara Maalumu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe:Said Soud Said akitoa salamu za serikali, kwa wanafamilia na wanajeshi wa JWTZ Kisiwani Pemba, juu ya kifo cha mpendwa wao MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, aliyefariki dunia wakati akiiwakilisha Tanzania katika ulinzi wa Amani Nchini DRC CONGO.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MEJA Laurence Salvatory Anatory akisoma wasifu wa marehemu, MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, aliyefariki dunia wakati akishiriki katika ulinzi wa Amani nchini DRC CONGO.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
LUTEENI kanali Benjamini Kingamkono kutoka kikosi cha 151 KJ Wawi Kisiwani Pemba, akitoa salamu za askari wa JWTZ Pemba wakati wa kuuwaga Mwili wa marehemu MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, aliyefariki dunia wakati alipokuwa akilinda amani nchini DRC Congo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
VIONGOZI mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na SMT, wakiongozwa na Waziri asiye na Wizara Maalumu za SMZ Said Soud Said, wakati wa kumuombea dua marehemu MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, aliyefariki dunia wakati akilinda amani nchini DRC CONGO.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MAKAMANDA mbali mbali wa ulinzi na Usalama, wakiitikia dua ya kumuombea marehemu MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, aliyefariki dunia akiwa katika majukumu yake ya kitaifa nchini DRC CONGO.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MMOJA wa Askari wa JWTZ Kisiwani Pemba, akitoa salamu zake za mwisho kwa marehemu MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, wakati mwili wake ulipofikishwa kijijini kwao kwa taratibu za mazishi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
KAMANDA wa Polis Mkoa wa Kusini Pemba Sheikhan Mohamed Sheikhan, akitoa salamu zake za mwisho kwa marehemu MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, wakali ulipowasili kijijini kwao Gombeume kwa taratibu za mazishi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
ASKARI wa Gwaride wakiwa wameubeba Mwili wa askari Mwenzao MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, kuupeleka nyumbani mwao kwa ajili ya taratibu za mashi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WANANCHI mbali mbali kutoka Vijiji jirani na Gombeume, wakiubeba mwili wa marehemu ndugu na kaka yao, MT94601 PTE Hamad Haji na kuupeleka katika msikiti kwa ajili ya kusaliwa na kupelekwa katika nyumba yake ya milele.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WANANCHI mbali mbali Kisiwani Pemba, wakiongozwa na Waziri asiye na Wizara Maalumu wa SMZ, Said Soud Said wakati wa kumsalia MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, kwa ajili ya kumpeleka katika makaazi yake ya mwisho.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

WAZIRI asiye na Wizara maalumu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Said Soud Said akitumba mchanga katika kaburi la MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, baada ya mwili wake kuzikwa kijijini kwao Gombeume Wilaya ya Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla, akitumba mchanga katika kaburi la MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, baada ya mwili wake kuzikwa kijijini kwao Gombeume Wilaya ya Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
ASKARI wa JWTZ Kisiwani Pemba, wakijiandaa kupiga risasi 21 kuashiria utoaji wa heshima ya utii, kwa askari mwenzao MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, baada ya taratibu za mazishi kumalizika akitumba mchanga katika kaburi la MT94601 PTE Hamad Haji Bakari, baada ya mwili wake kuzikwa kijijini kwao Gombeume Wilaya ya Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.