Habari za Punde

Rais Dk Shein awaapisha viongozi aliowateua karibuni

 
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
 Zanzibar                                 07.12.2017

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewaapisha Wakuu wa Mikoa wapya pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto (anaeshughulikia masuala ya Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto),viongozi ambao aliwateua hivi karibuni kushika nyadhifa hizo.

Viongozi walioapishwa hivi leo katika ukumbi wa Ikulu mjini Zanzibar ni Hassan Khatib Hassan kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hemed Suleiman Abdalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba na Mwanajuma Majid Abdalla kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto (anaeshughulikia masuala ya Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto).

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Mawaziri na Manaibu Waziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee.

Wengine ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa Zanzibar, Wakuu wa Vikosi vya SMZ, pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.