Habari za Punde

Watumishi watakiwa kujiepusha na Kujihusisha na Ubadhirifu wa Mali na Rushwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Wakili Said Chiguma akielezea weledi wa wahitimu wa Chuo hicho unaosababisha wengi kupata taaluma ya juu ya Uhasibu- CPA wakati wa Mahafali ya 15 ya Chuo hicho kwa Kampasi ya Mtwara na Dar es Salaam, yaliyofanyika  Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza na wahitimu wa Kozi mbalimbali katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania – TIA kuhusu kujiepusha na masuala ya Rushwa wawapo kazini wakati wa Mahafali ya 15 ya Chuo hicho kwa Kampasi ya Mtwara na Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahitimu wa Kozi mbalimbali wa katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania-TIA Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara, wakisubiri kwa hamu kutunukiwa shahada zao katika Mahafali ya 15 ya Chuo hicho kwa Kampasi ya Mtwara na Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa tatu kushoto) akiwa amejiunga na  viongozi wengine wa Taasi ya Uhasibu Tanzania na wahitimu kupata burudani ya muziki muda mfupi baada ya kuwatunuku vyeti katika  Kozi mbalimbali Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ( kushoto)  akimpa zawadi Bw. Fransis Levis Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo yake katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa Shahada ya Kwanza katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania – TIA wakiwa na furaha baada ya kutunukiwa vyeti vya Kozi mbalimbali na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto)  akimpa mkono wa pongezi Mhitimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Kampasi ya Mbeya Bw. Ambwene Mwasongwe aliyefika katika Mahafali ya Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam akiwakilisha wenzake baada ya kutumbuiza kwa wimbo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa tatu kushoto) na meza Kuu wakiimba Wimbo wa Taifa ikiwa ni ishara ya kuhitimisha kwa mahafalli ya 15 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania – TIA Kampasi ya Mtwara na Dar es Salaam Jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ( katikati), Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania- TIA, Dkt. Joseph Kihanda (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Taasisi hiyo Wakili Said Chiguma wakielekea katika Ofisi za Taasisi hiyo baada ya kuhitimisha mahafalli ya 15 ya Taasisi hiyo kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasi.iano Serikalini Wizara ya GFedha na Mipango) 

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Ashatu Kijaji,  amewataka wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kujiepusha na vitendo vya rushwa na ubadhilrifu wawapo kazini na badala yake wafanye kazi kwa bidii, uadilifu, umakini kwa kuzingatia Sera, sheria, kanuni  na taratibu za kitaaluma zilizowekwa.

Dkt. Kijaji aliyasema hayo wakati akiwatunuku vyeti vya kozi mbalimbali wahitimu 3,538 wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania- TIA, wakati wa mahafali ya 15 ya Chuo hicho kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara, Jijini Dar es Salaam.

‘Vitendo vya rushwa na  ubadhirifu vina madhara makubwa kwa maisha ya mtu mmoja mmoja na uchumi wa Taifa letu kwa ujumla, ni vyema kila wakati mkumbuke kuwa rushwa ni adui wa haki na maendeleo ya Taifa.’ Alieleza Dkt. Kijaji.

Aliwataka Wahitimu wa Taasisi hiyo kujielekeza katika kujiajiri na kuajiri wengine kutokana Soko dogo la ajira hasa ajira rasmi ambalo halikidhi mahitaji ya wahitimu wote nchini.

‘Hatua mliyofikia iwe chachu ya kujiimarisha zaidi kitaaluma ili kuweza kushindana katika soko la ajira na kujiajiri bila kufanya hivyo kazi nyingi za ndani zitachukuliwa na wageni kutoka nje’, alisisitiza Naibu Waziri Kijaji.

Alisema kuwa TIA ni miongoni mwa Taasisi za Elimu ya Juu nchini zinazotoa mafunzo kwa viwango vya kimataifa hivyo ni vyema kuendeleza mafanikio yaliyopatikana bila kusahau kuboresha mahali palipo na mapungufu.

Dkt. Kijaji alisema kuwa fani za Uhasibu ikiwemo Uhasibu wa Fedha za Umma, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Biashara, Uongozi wa Raslimali Watu na Masoko ni muhimu  katika kuendesha uchumi wa viwanda, hivyo umahiri wa wataalamu wanaozalishwa katika taasisi hiyo unatakiwa kuonekana katika kukabiliana na changamoto za usimamizi wa mapato na matumizi ya fedha za umma, mahitaji ya Soko, ushindani na utandawazi.

Taasisi ya TIA imetakiwa kuendelea kuboresha mitaala ili kukidhi viwango vya kimataifa kwa kuwa Dunia ya sasa ni ya teknolojia hivyo kama Taasisi inatakiwa kuendana na teknolojia hiyo ambayo itasaidia kubadilishana maarifa.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dkt. Joseph Kihanda alisema kuwa kati ya wahitimu 3,538 wanawake ni 1,846 sawa na asilimia 52.2 na wanaume ni 1,692 sawa na asilimia 47.8. Wahitimu 233 ni wa Kampasi ya Mtwara na wahitimu 3,305 ni wa Kampasi ya Dar es Salaam.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Taasisi hiyo Wakili Said Musendo Chiguma alisema kuwa kwa  miaka miwili mfululizo kuanzia mwaka 2015/2016 na 2016/2017 Taasisi hiyo imeongoza kwa kutoa wafaulu wengi wa shahada za juu ya taaluma ya Uhasibu- CPA na taaluma ya Ugavi- CPSP ambapo kwa kipindi cha miaka mitano imetoa asilimia 10 ya wahitimu wote kitaifa.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amewapongeza Wahitimu wote kwa jitihada walizozifanya hadi kufikia hatua hiyo ya kupata vyeti japokuwa amewahimiza kujiendeleza zaidi kitaaluma ili kuongeza weledi.

Imetolewa na:
Benny Mwaipaja
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
15 Desemba 2017

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.