Habari za Punde

Zanzibar Heroes Yapongezwa na Kuzawadiwa Fedha Na Viwanja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud akimsalimia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, baada ya kuwasili katika viwanja vya Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo kujumuika na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanziba Heroes wakati wa Chakula cha Usiku alichowaandalia Mashujaha wa Zanzibar Heroes kwa hatua waliyofikia katika Michuano ya Kombe la Chalenji Nchini Kenya na kushika nafasi ya Pili ya Michuano hiyo baada ya kufungwa katika Mchezo wa Fainali na Timu ya Taifa ya Kenya kwa matuta 3 - 2. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali. Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar. kuhudhuria hafla aliyowaaandalia Wachezaji wa Timu ya Zanzibar Heroes katika ukumbi huo na kuwazawadia. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, alipowasili katika ukumbi wa hafla ya chakula cha usiku alichowaandalia Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes na kuwakabidhi zawadi alizowaahidi wakati wa chakula cha mchana cha kuwapongeza kilichofanyika Ikulu Zanzibar juzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakiwa wamesimama wakati ukiimbwa wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya chakula maalum kwa Wachezaji wa Zanzibar Heroes katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar.
Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar kikipiga wimbo wa Taifa wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes kwa ushindi wao katika michuano ya Kombe la Chalenji kwa kufika hatua ya Fainali ya Michuano hiyo iliofanyika Nchini Kenya wiki iliopita.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes wakiwa wamesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya chakula cha usiku na kuzawadia zawadi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein. Katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes wakiwa wamesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya chakula cha usiku na kuzawadia zawadi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein. Katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar.
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Moroco akiwatambulisha wachezaji wa Timu yake kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, wakati wa hafla ya chakula cha usiku walioandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza na kuzawadia zawazi kwa hatua walioonyesha katika Michuano ya Kombe la Chalenji Nchini Kenya wiki iliopita.












No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.