Habari za Punde

Abdul Aziz Makame kujiunga na Sofapaka ya Kenya



Mchezaji kiungo mchezeshaji wa Jang'ombe yupo mbioni kusajiliwa na Timu ya Sofapaka ya Kenya.

Abdul Aziz ambae aliitumikia vyema Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes katika mashindano ya CECAFA yaliyomalizika karibuni huko Machakos nchini Kenya alionyesha kiwango kizuri cha soka pamoja na uwezo wa kufunga mabao na kutoa pasi za uhakika.

Kiungo AbdulAziz ambae ana umri wa miaka 21 anasubiri kumalizana kati ya timu yake ya Jang'ombe na Sofapaka lakini mwenyewe yupo tayari kujiunga na timu hiyo ya Kenya wakati wowote.

Abdul Aziz Makame anakuwa mchezaji wa pili wa Zanzibar Heroes kuwaniwa na Timu za Kenya baada ya Beki wa Yanga, Mwinyi Haji Ngwali ambae anatakiwa na Timu ya Leopards ya Kenya pia.

Pia anakuwa mchezaji wa tano wa kigeni wa Timu ya Sofapaka ambae anatarajiwa kusajiliwa katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.