Habari za Punde

Balozi Seif akabidhi vifaa vya michezo kwa timu 14 jimbo la Chumbuni

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif akikabidhi vifaa vya Michezo kwa Mwakilishi wa Timu ya Soka ya G.S ya Shehia ya Karakana.
 Balozi Seif akimkabidhi Seti ya Jezi na Mipira Miwili Mwakilishi wa Timu ya Soka ya Chumbuzi City kwenye Mkutano wa Majumuisho hapo chuop cha Utalii Maruhubi.
  Balozi Seif akimkabidhi seti ya Jezi na Mipira Miwili Mwakilishi wa Timu ya Soka ya F.C Muembe Makumbi United.
Mwakilishi wa Timu ya Soka ya F.C Jupiter iliyomo ndani ya Jimbo la Chumbuni akipokea Seti ya Jezi na Mipira Miwili kutoka kwa Balozi Seif vilivyotolewa na Uongozi wa Jimbo la Chumbuni.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amekabidhi vifaa vya michezo kwa Timu 14 za mchezo wa Soka  za Jimbo la Chumbuni vilivyotolewa na Uongozi wa Jimbo hilo vikilenga kuimarisha Sekta ya michezo kwa vijana wa eneo hilo.

vifaa hivyo ni miongoni mwa ahadi za Viongozi hao waliyoitowa wakati wa kampeni za uchaguzi kuelekea katika mnasaba wa kutekeleza vyema ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015/2020.

Balozi Seif alikabidhi vifaa hivyo wakati akimaliza ziara yake ya kutwa moja katika Jimbo la Chumbuni kwenye Mkutano wa Majumuisho uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Vifaa hivyo vinavyokadiriwa kugharimu zaidi ya shilingi Milioni Tatu ni pamoja na Seti ya Jezi na Mipira Miwili kwa Timu Tano kwa niaba ya nyengine 14 zilizomo ndani ya Jimbo hilo.

 Akizunumza na wanajimbo hao Balozi Seif  ameupongeza mshikamano mkubwa unaoendelea kutawala ndani ya Jimbo la Chumbuni ambao unapunguza changamoto zinazowakabili watu wake.

Akitoa Taarifa katika Mkutano huo wa Majumuisho  Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza Maarufu Amjadi alisema Timu zote 14 za Soka kwenye Jimbo hilo tayari zimeshapata usajili wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar {ZFA}.

Amjadi alisema Uongozi wa Jimbo hilo utaendelea kuzihudumia Timu hizo katika masuala ya usajili. Vifaa pamoja na uwezeshaji ili zinapoingia kwenye mashindao ziweze kushinda badala ya kushiriki.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.