Habari za Punde

Mamlaka za Usafirishaji za SMT na SMZ Zakutana.

 Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyekiti Mwenzake Mwenza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakikiendesha Kikao cha Serikali za SMT na SMZ kuzungumzia kadhia meli za Kimataifa zinazofanya biashara haramu ambazo zimepata usajili Tanzania.
Kikao hicho kilichohusisha pia watendaji wa Mamlaka zinazosimamia masuala ya Usafiri wa Baharini kilifanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyekiti Mwenzake Mwenza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakiagana baada ya kumalizika kwa mazungumzo ya Kikao cha Serikali za SMT na SMZ kuzungumzia kadhia meli za Kimataifa zinazofanya biashara haramu ambazo zimepata usajili Tanzania.

Kikao hicho kilichohusisha pia watendaji wa Mamlaka zinazosimamia masuala ya Usafiri wa Baharini kilifanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Na.Othman Khamis OMPR.

Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu  Hassan kesho anatarajiwa kutoa Taarifa Rasmi ya Serikali kuhusu sakata la Meli zilizokumbwa na matukio mbali mbali ya kusafirisha bidhaa zilizo kinyume na matakwa ya Umoja wa Mataifa ambazo zinapepea Bendera ya Tanzania.

Hatua hiyo ya  Serikali ya Muungano inatokana na kusikitishwa kwake  na baadhi ya Taarifa zinazoendelea kuenea katika vyombo mbali mbali vya Habari  ndani ya Nje ya Nchi pamoja na Mitandao ya Kijamii  juu ya kuchafuliwa sifa yake katika Jumuiya za Kimataifa.

Taarifa ya Mh. Samia imekuja kufuatia Kikao cha pamoja cha Mawaziri na Watendaji wa Mamlaka zinazosimamia Usafiri wa Baharini wa Serikali zote Mbili alichokiongoza akiwa na Mwenyekiti Mwenza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 
Balozi Seif Ali Iddi kilichofanyika Vuga Mjini Zanzibar.

Makamu wa Rais atatumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi juu ya hatua zitakazopaswa kuchukuliwa na Tanzania  katika kukabiliana na matukio hayo kutokana na usajili wa Meli za Kimataifa unaofanywa  na Mamlaka ya Usafiri wa  Baharini Zanzibar {ZMA}.

Wajumbe wa Kikao hicho mbali ya kujadiliana kadhio hiyo pia walipata fursa ya kupanga mikakati ya muda mrefu itakayoiwezesha Tanzania kupitia vyombo vinavyohusika na usimamizi wa usajili kubuni mbinu za kuondosha kabisa matatizo yanayojitokeza.

Hivi karibuni yapo matukio ya Meli zilizokuwa zikifanya biashara haramu na kusajiliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar {ZMA} huku zikipeperusha Bendera ya Tanzania jambo ambalo Tanzania haikubali liendelee kutokea.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.