Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk. Shein Atembelea Kisiwa na Utalii Cha Al Marjan Nchini Ras Al Khaimah.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mkurugenzi wa Kisiwa cha Utalii cha Al Marjan Ras Al Khaimah, Abdullah Al Abdouli wakitembelea katika moja ya Hoteli zilizo jengwa katika kisiwa hicho cha Kitalii Nchini Ras Al Khaimah. Rais wa Zanzibar akiendelea na ziara yake katika Nchi za Falme za Kiarabu UAE.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mama Mwanamwema Shein na Viongozi wa Serikali wakipata maelezo ya picha ya majengo ya mahoteli ya Kitalii yaliojengwa katika eneo la kisiwa  hicho cha Al Marjan Nchini Ras Al Khaimah kulia Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Kisiwa cha Al Marjan Abdullah Al Abdouli, wakisikiliza maelezo ya picha za majengo yaliojengwa katika kisiwa hicho.
MOJA ya majengo ya Mahoteli ya Kitalii yaliojengwa katika eneo hilo ka kisiwa hicho cha Al Marjan Nchini Ras Al Khaimah kama linavyoonekana


UJUMBE wa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakitembelea moja ya hoteli ya kitalii katika Kisiwa cha Kitalii cha Al Marjan Nchini Ras Khaimah katika ukanda wa kisiwa hicho

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.