Habari za Punde

Wizara ya Elimu yanyooshewa kidole upotevu wa Milioni 145 kwa uzembe

Na Ali Issa, Maelezo   

Tafiti ya mkaguzi mkuu wa mfuko mkuu wa hesabu za serikali umegundua kasoro katika wizara ya elimu na mafuzo ya amali wizara ya Afya Zanzibar kupotea pesa za serikali kwa uzembe wa baadhi ya waliopewa dhamana katika sehemu zao za kazi kushindwa kuwajibika.

Hayo yamesemwa leo huko Ikulu Zanzibar na katibu mkuu kiongozi, Abdulhamid Yahya Mzee wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini hapo.

Alisema kumekuwa na uzembe pale ambapo mtumishi wa umma anapostaafu, kwenda likizo bila malipo, pesa za serikali kuendelea kupokewa mishahara hewa kwa watu ambao hawaesabiki tena kupokea mishahara kazini na kuendelea kulipwa kitu ambacho ni tatizo.

Amesema katika ukaguzi uliokuwa ukifanywa katika wizara ya elimu na mafuzo ya amali imegunduliwa zaid ya milioni 145 zililipwa kwa watu waliokuwa wamestaafu na waliochukua likizo bila malipo kitu ambacho hawakustahiki kuchukua pesa hizo.

Amesema jambo hilo lilitokea kwa uzembe kwa taasisi tatu ambapo ni, Wizara ya elimu, Utumishi wa umma na utawala bora na Wizara ya Fedha kwani wao ndio wana mamlaka hayo ya ushirikiano kwa mfanya kazi juu ya kustaafu na mishahara yake.

“Mtafiti aligundua zaidi ya milioni 145 ziliingizwa kaitka mishahara kwa watu waliokuwa hawastahiki kulipwa na baadhi yao wametumia ”,alisema katibu kiongozi.

Aidha alisema kuwa pesa hizo walilipwa watu 46 ambao kati yao walikuwa wamestaafu na kuchukuwa likizo bila malipo kutokuwepo nchini kwa mambo yao binafsi na pesa hizo kupokewa na jamaa zao.

“Wizara ya elimu walikuwa jumla ya watu 46 ambao hawakustahiki kulipwa walipokea pesa hizi”aliongeza kusema katibu.

Hata hivyo katibu huyo alisema kuwa watu hawo wamegundulikana waliochukuwa pesa hizo ijapokuwa alishindwa kuwataja na kusema kuwa baadhi yao wamerejesha pesa hizo na kilicholipwa  hadi sasa kufikia zaidi milioni 82 ,wapo waliomaliza na wengine wanaendelea kulipa.

Pia katibu alisema kuwa kwa upande wa wizara ya Afya iligundulika kesi moja ya mtu aliosaini mshahara wa wa daktari mgeni kutoka  Nchini Cuba  ambaye alikuwa ameshondoka kwa kumaliza muda wake, lakini mtu huyo alithubutu kutia saini na kuchukua mshahara kitu hicho ni kosa kwa mfanyakazi na mtu huyo atachukuliwa hatuwa za nidhamu.

Alisema kwa upande wa wizara ya kilimo marejesho ya utafiti hayakubaini kasoro kwani waliokuwa hawaonekani baadae waligundulikana kuwa wako masomoni nje ya nchi mtafiti mkuu wa hesabu za serikali aliridhika.

Katibu alisema pamoja na yote hayo wapo wafanyakazi 28 ambao wamefukuzwa kazi wizara ya kilimo kwa makosa hayo na watachukulia hatuwa kali wote walioingia hatiani kusababsha upotevu wa fedha za serikali kizembe. 

Katbu aliwataka watumishi wenye mamlaka kuwajibika kwa nidhamu juu upotevu wa fedha za serikali na sasa wanamalizia uchunguzi unaofanywa na baadae hatua zitachukuliwa kwa watu hao

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.