Habari za Punde

MKIKITA WAFURAHIA HUDUMA NZURI SPICE HOTEL LIMITED DAR

 Viongozi wa Mtandao wa Kijani kibichi Tanzania (Mkikita), wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Kissui Steven Kissui (Kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao huo, Adam Ngamange (wa nne kushoto), wakiwa nje ya  Spice Hotel Limited,  baada ya kufanya mkutano na waandishi wa habari hoteni hapo, Dar es Salaam jana.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Uongozi wa Mkikita umefurahishwa na huduma za hoteli hiyo iliyopo makutano ya mitaa ya Narung'ombe na Lumumba Karikaoo Dar es Salaam na kuahidi mikutano mingine ijayo kuendelea kufanyia hapo.

Baada ya kumaliza mkutano, uongozi wa Mtandao huo ulimtembelea Mmiliki wa Hoteli Ofisi kwake, Bw. Mwangaba kwa lengo la kufahamiana pamoja na kumpa pongezi kutokana na hoteli hiyo kuwapatia huduma nzuri.

Mwangaba mwenye hoteli hiyo ya kisasa yenye vyumba 67 vyenye hadhi tofauti alishukuru na kuwakaribisha tena kwenda hapo kwa shughuli mbalimbali. Pia alikubali kujiunga na mtandao ili awe anashiriki kwenye shughuli mbalimbali zinazofanywa na mtandao huo na kunufaika nazo pia. Kwa habari zaidi kuhusu hoteli hiyo soma maelezo yaliyopo mwisho wa ukurasa huu.
 Hoteli yenyewe
 Viongi wa Mkikita wakiwa katika picha ya pamoja na Mmiliki wa Hoteli ya Spice, Mwangaba (wa pili kushoto). Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi,  Dk. Kissui S. Kissui, Meneja wa Mashamba, Catherina, Ofisa wa Logistic, Morris Mwita, CEO Adam Ngamange, Ofisa Uhusiano, Neema Fredrick na Meneja Masoko, Deo.
 CEO Adam Ngamange akizungumza katika mkutano na wanahabari, kuhusu maandalizi ya mafunzo ya kilimo biashara cha Papai Salama kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All, Askofu Edger Mwamfupe akizungumza kuhusu makubaliano ya ushirikiano waliosaini na Mkikita kwa lengo la kuwakomboa wananchi masikini Tanzania.
 Mfanyabiashara Adamjee akielezea jinsi anavyokiendesha kwa faida kubwa kilimo cha pilipili kichaa
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui akizungumza katika mkutano huo, kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na mtandao huo.
 Ofisa Uhusiano wa Mkikita, Neema, akielezea utaratibu unaotumika kuwasajili watu wanaotaka kuhudhuria mafunzo ya kilimo kibiashara cha Papai Salama
 Mmiliki wa Spice Hotel, Mwangaba (kulia), akizungumza alipokutana na viongozi wa Mkikita kwa lengo la kufahamiana
 Mwangaba akiagana na Adam Ngamange
 Mwangaba akiagana na Catherina
Mwangaba akiagana na Dk. Kissui

Spice hotel is a first class property located at Lumumba /Narung'ombe Street.

The hotel has 67 Rooms, including single 47, Deluxe/ Suites 6 and Double 14 with a view to the north and South of the city.

 The perfect services and highly qualified staff will make your staying here comfortable. 

Every receptionist knows more than one language. A warm heaven reception awaits you at our new Spice hotel. 

Spice hotel has just been opened; we bring to you standards found in Spice hotel right at your door steps. 

We are committed to offer a true value of money experienced in an environment of unique d?cor, peace and comfort. 

Accommodation Our rooms are of high quality and conditioned equipped with TV (DSTV & Satellite channels), hot water system, refrigerators, minerals water, free internet Access etc, to mention but a few, security within the building is superb 24hrs with electronic camera security. We do offer conference facilities for up to

Anwani ya Biashara
Ilala, Kariakoo Dar Es Salaam
Lumumba /Narung'ombe Street Opposite Mnazi Mmoja Ground

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.