Habari za Punde

Mbio za Nusu Marathoni yafana Zanzibar

Washiriki kutoka ndani na nje ya nchi wakitoana jasho katika mashindano ya nusu Marathoni yaliyofanyika leo 


Washiriki kutoka ndani na nje ya nchi wakitoana jasho katika mashindano ya nusu Marathoni yaliyofanyika leo 
Mshindi wa mashindano ya Nusu Marathoni kwa upande wa wanawake Angel Juma akimaliza mbio hizo
Washiriki wa Nusu Marathoni waliojitokeza kushiriki mashindano hayo walipokuwa wakianza mbio hizo Ngome Kongwe
Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Mashindano ya Zanzibar Half Marathon yamefanyika leo hii Foradhan Mjini Unguja huku wanariadha zaidi ya 500 kutoka nchi mbali mbali walishiriki Mashindano hayo kwa kilomita 5, 10 na 21.
Mashindano hayo yaliyofanyika kwa mara ya kwanza Zanzibar  yalianzia katika  ukumbi wa Ngome Kongwe Forodhani  na kupitia maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar  ikiwa ni katika kuhamasisha  kupiga vita vitendo vya udhalilishaji kwa  watoto na wanawake zanzibar.

Akizungumzia Mashindano hayo Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Zanzibar, Abdul Hakim Cosmas Chasama amesema Mashindano hayo yamewapa mazoezi mazuri wanaridha ambao watashiriki Mashindano mbali mbali makubwa yakiwemo ya ndani na nje ya Tanzania.

Mshindi wa kwanza Kilomita 21 Wanaume amefanikiwa kuwa Dickson Marwa kutoka Tanzania Bara huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Mohammed Ramadhan Mgeni kutoka Zanzibar huku nafasi ya tatu ikikamatwa na Remigius John kutoka Tanzania bara.

Kwa upande wa Wanawake Kilomita 21  Angel John Juma kutoka Tanzania bara ameshika nafasi ya kwanza  huku nafasi ya pili ikikamatwa na Asma Rajab kutoka Zanzibar wakati nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mia Vejlgaard Just kutoka Denmark.

Na katika kilomita 10 Wanaume mshindi ni Abdallah Jecha Abdallah kutoka Zanzibar, mshindi wa pili ni Filipo Jacob Mambo kutoka Tanzania bara huku Said Khamis Ali kutoka Zanzibar akishinda nafasi ya tatu.

Wanawake kilomita 10 washindi ni Rosemery Gustaph Malki kutoka Tanzania Bara huku nafsi ya pili ikikamatwa na Warda Shaaban Mbura kutoka Zanzibar na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Maria Michael Benedictor kutoka Tanzania bara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.