Habari za Punde

BITEKO AWAPA SHAVU WANAWAKE BUKOMBE ASEMA HAWAPASWI KUBEZWA KAMA ILIVYO DESTURI NA MTAZAMO WA WENGI

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Madini akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe, Leo 8 Machi Machi 2018. Picha Zote Na MathiasCanal-Wazo Huru Blog
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Madini (Kushoto) akijadili jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe, Leo 8 Machi Machi 2018. 
Maandamano ya wanawake wakielekea katika dhifa ya maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe, Leo 8 Machi Machi 2018. 
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Madini akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe, Leo 8 Machi Machi 2018.

Na Mathias Canal, Bukombe-Geita
Mwanamke si mtu wa kubezwa kama ilivyo desturi na mtazamo wa wengi kwamba mwanamke hawezi kufanya jambo lolote kama hatawezeshwa, Hii ni dhana mfu tena iliyopitwa na wakati tumejionea wanawake wangapi ambao wanawawezesha wanaume tena bila hata wao kuwezeshwa.

Hayo yamesemwa  Leo 7 Machi 2018 na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Madini wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe na kusisitiza kuwa watanazania hawapaswi Kuishi kwa kukariri ni hatari kwa ustawi wa maisha yetu hivyo ni vyema kama tutaishi kwa kujifunza maana hata tafsiri ya maisha nyepesi ni ile ya kuishi na kujifunza.

Alisema kuwa Katika Jamii mara kadhaa yameripotiwa matukio mbalimbali ikiwemo yale ya kuwanyanyapaa wanawake, kuwapiga lakini yapo pia matukio ovu kabisa ya kuwabaka wanawake jambo ambalo Serikali inaendelea na juhudi za makusudi kukomesha madhila hayo.

"Mwanamke ana heshima kubwa ya Jinsia yake lakini pia Wanawake ni mama zetu, dada zetu, wake zetu, wadogo zetu, shemeji zetu, shangazi zetu lakini pia ni Nyanya (bibi) zetu" Alikaririwa Mhe Biteko na kuongeza kuwa

Kauli mbiu ya siku ya wanawake mwaka 2018 isemayo “Kuelekea uchumi wa viwanda tuimarishe usawa wa kijinsia na uwazeshaji wa wanawake vijijini” inasisitiza kuwajengea wanawake uwezo wa kitaaluma, Kibiashara, Upatikanaji wa mitaji, Masoko na Mikopo ili waweze kushiriki kwa usawa na kunufaika na fursa zilizopo badala ya kuwa wasindikizaji tu.

Maadhimisho ya wanawake Duniani hufanyika kila mwaka ifikapo Machi 8, ambapo inaelezwa kuwa maadhimisho hayo ya siku ya wanawake Duniani kwa mara ya kwanza yalifanyika Februari 28, 1909 huko Marekani.

Umoja wa Mataifa wenyewe umesema siku hii ni ya kutafakari juu ya hatua za kimaendeleo ambazo wanawake wamepiga, kupongeza juhudiza wanawake wa kawaida kutokana na mchango wao katika historia ya maendeleo ya nchi na jamii zao.

Mbunge huyo wa Bukombe Mhe Biteko alisisitiza kuwa maadhimisho hayo yaifanya kuwa siku ambayo wanawake hutambuliwa kwa mchango na mafanikio yao bila kujali mipaka ya kitaifa, rangi, lugha, utamaduni, uchumu wala siasa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.