Habari za Punde

Siku Msanii Maarufu wa Muziki wa Bongo Flava Alipowasili Katika Viwanja Vya Zamani Vya Baraza la Wawakilishi Kukabidhiwa Hati ya Usajili wa Vituo vya TV na Redio Wasafi Zanzibar.

Msanii Maarufu Nchini Tanzania Nasib Daimond akiwasili katika viwanja vya Zamani vya Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar kuhudhuria hafla ya kukabidhiwa Hati zake za Usajili wa Kituo cha TV na Redio Wasafi na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar. Mhe. Rashid Ali Juma. Wasafi TZna Redio zimesajiliwa Zanzibar kwa kutowa burudani na Elimu kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania.
Wasanii Muziki wa Bongo Flava Tanzania wakimsindikiza MsaniiNasib Daimond katika hafla ya kukabidhiwa Hati ya Usajili wa Vituo vya Redio na TV ya Wasafi Zanzibar wakielekea katika ukumbi wa mkutano wazamani waBaraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar wiki iliopita.
Wasanii wa Muziki wa Bongo Flava Tanzania wakiwa na Msanii Maarufu Tanzania Nasib Diamond wakiwa katika ukumbi wa zamani baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar wakihudhuria hafla ya kukabidhiwa hati ya usajili wa Kituo cha Redio na TV Wasafi.. 
Kaimu Katibu Mtendaji Mamlaka ya Utangazaji Zanzibar (ZBC) Chande Omar akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Haji ya Usajili ya Vituo vya Utangazaji vya Wasafi Redio na TV, vinavyomilikiwa na Msanii Maarafu Tanzania Nasib Diamond.kushoto Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo. Zanzibar Dkt.Juma Mohammed.
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Hati ya Usajili ya Vituo vya Utangazaji vya Wasafi TV na Redio hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar.






2 comments:

  1. Zanzibar imekwisha zamani wakikaribishwa mashekhe wakubwa Leo tunakaribisha wasanii wazidi kupotosha kizazi chetu, tusubiri gharka tu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ndio lililo bakia

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.