Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ziarani Nchini Cuba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa kuelekea Nchini Jamuhuri ya Cuba kwa ziara Maalum.

Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Mh.Mahmoud Thabit Kombo akimtakia safari njema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anayeelekea Nchini Cuba kwa ziara Maalum.

Picha na – OMPR – ZNZ.Na. Othman Khamis OMPR.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameondoka Zanzibar leo mchana kupitia Mjini Dar es salaam kuelekea  Nchini Jamuhuri ya Cuba kwa ziara Maalum.Katika ziara hiyo Balozi Seif  ameondoka  Nchini akifuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pamoja na baadhi ya wasaidizi wake.Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar Balozi Seif aliagwa na baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu wa SMZ, Watendaji wa Serikali pamoja na Viongozi wa Vyama vya Kisiasa viliopo  hapa Nchini.Ziara ya Balozi Seif  Nchini Jamuhuri ya Cuba pamoja na mambo mengine atapata fursa ya kuwatembelea baadhi ya Madaktari Wazalendo wa Zanzibar wanaoendelea kupata Mafunzo yao ya ngazi ya juu ya Shahada ya
Uzamili ya Udaktari.Madaktari hao Wanane wa Awamu ya kwanza ni kati ya wale 15 walioteuliwa kupata mafunzo ya juu Nchini Cuba  ikiwa ni miongoni mwa waliomaliza mafunzo yao kupitia Mpango Maalum wa masomo ulioasisiwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Cuba na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Ziara hiyo Maalum ya Balozi Seif  imelenga kuendeleza ushirikiano wa Kihistoria wa muda mrefu uliopo kati ya Jamuhuri ya Cuba pamoja na Zanzibar hasa katika Sekta ya Afya ambayo zimeleta mafungamano ya Nchi
hizo rafiki Kisiasa na Utamaduni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.