Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Azungumza na Ujumbe wa Kampuni ya ZTE Leo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sewif Ali Iddi wa Tatu kutoka Kushoto akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Mtandao wa Mawasiliano ya Kisasa ya China ya ZTE Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Rais wa Kampuni ya ZTE Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Bwana Darren Zhao kati kati akisisitiza jambo wakati ujumbe wake ulipofanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa ZanzibarBalozi Seif.Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Zanzibar 
Balozi Seif  Rais wa Kampuni ya ZTE Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Bwana Darren Zhao akimkabidhi Balozi Seif zawadi Maalum kutoka kwa Uongozi wa Kampuni yake ya ZTE.
Balozi Seif akimkabidhi Bwana Darren Zhao zawadi ya Mlango wa Zanzibar kama ishara ya kuifungulia mlango zaidi wa uwekezaji Kampuni ya ZTE Visiwani Zanzibar.

Na.Othman Khamis OMPR.
Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana kwa mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Mtandao wa Mawasiliano ya ZTE wenye Makao Mkuu yake Nchini Jamuhuri ya Watu wa  China ulioongozwa na Rais wake Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika.

Katika mazungumzo yao Balozi Seif aliishukuru na kuipongeza Kamuni ya ZTE kwa kufanikisha uwekaji wa Mkonga wa Taifa Awamu ya Kwanza kazi ambayo imekamilika Mnamo Mwaka 2012 kazi ambao itakuwa kichocheo muhimu katika kuimarisha sekta ya huduma za Uchumi na kuongezeka kwa mapato ya Serikali.

Akizungumzia awamu ya Pili ya uwekaji wa Mkonga wa Taifa ambao umeelekea zaidi katika huduma za Kijamii na Kiserikali kupitia mfumo wa Mtandao wa Kisasa E- Government, E – Health na E – Tax alisema mabadiliko makubwa yameanza yameanza kupatikana.

Balozi Seif alisema mashine za Kisasa tayari zimeshafungwa ikiwemo MRI na kuanza kutoa huduma  kwa Wananchi katika Sekta ya Afya ambapo kabla walilazimika kuzifuata huduma hizo nje ya Zanzibar na kutumia gharama kubwa.

Kuhusu mfumo wa ukusanyaji wa Mapato kwa njia ya mtandao ambapo ZTE inaendelea na mazungumzo yake na Bodi ya Mapato Zanzibar Balozi Seif alisema angependa kuona  Mfumo huo { E – Tax } unafanya kazi Zanzibar ili Serikali ijitosheleze kimapato.

Alisema uzoefu unaonyesha wazi kwamba Mfumo huo wa E – Tax unapotumika vizuri mapato ya Taifa huongezaeka kutokana na kudhitiwa vyema ukusanyaji wake sambamba na maisha ya Wananchi wake kutengemaa.

Naye kwa upande wake Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Mtandao wa Mawasiliano ya ZTE Bwana Darren Zhao alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba ZTE imeongeza uwezo wa Kitaalamukatika kuona huduma wanazotoa zinakwenda na kasi ya KiduniaKimtandao.

Bwana Darren aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano wake uliyoiwezesha Kampuni hiyo kuendelea kutoa huduma zake  Tanzania na Zanzibar jkwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.