Habari za Punde

WanaCCM Pemba watakiwa kutembea kifua mbele na kuhakikisha CCM inajipanga kwa ushindi


Na Salmin Juma, Pemba

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ taifa Samia Suluhu Hassan, amewanyoosha wanacccm kisiwani Pemba, kwamba waanche kujinywezwa mithili ya kobe, wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu, jambo linalowapa fursa vyama vya upinzani kushinda.

Alisema uchangamfu walionao baada ya uchaguzi lazima wauoneshe wakati wa uchaguzi na watembee kifua mbele bila ya waoga wala wasiwasi wowote, na kuhakikisha chama kinashinda.

Mjumbe huyo wa Kamati kuu ya CCM taifa, alieleza hayo jana Tawi la CCM Ole wilaya ya Chakechake kisiwani humo, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la tawi hilo, ikiwa ni sehemu ya zaira yake ya siku tatu  kisiwani Pemba.

Alisema ndani ya CCM wapo waliokuwa hawana hamasa na kujinywezwa na kuonekana kama CCM haipo kwenye jimbo la Ole na maeneo mengine kisiwani Pemba, na kusahau kuwa wao taifa kubwa.

Alisema wanaccm wamekuwa waoga na kuogopa kung’ariwa na wapinzani na kisha viapo wanavyokula vya kukulinda chama havina ukweli na nia thabiti ndani yake.

Alisema, lazima vijana wa CCM wajenge ujasiri na uthubutu wa kweli na kujiamini katika kukilinda chama na kuongeza idadi ya wanachama wapya kila siku.

“Nyinyi ndio wale wanaccm mnaowatenga mwenzenu kwa sababu ya kuzungumza na mtu anaefikiriwa kuwa ni cha cha upinzani, jamani siasa hizo zimekwisha,”alisema.’

Katika hatua nyengine Mjumbe huyo wa Kamati kuu ya CCM taifa, alisema lazima matawi ya CCM yatumike katika kuongeza idadi ya wanachama wapya ili CCM kiendelee kushika hatamu.

Kuhusu wanaccm wanawake, Samia aliwataka kutekeleza kwa vitendo nyimbo za umoja na mshikamano wanazoziimba, na sio kusema kwa mdomo pekee bali iwe na kwa vitendo.

Alieleza kuwa, nyimbo kama ‘vigumu kutoka madarakani au tutaipigania kw anguvu zatu zote’ alisema lazima wajipange vyema kivitendo na kuhakikisha wanajitathimini na kama hawakubadilika wanaweza kutolewa
madarakani.

Kuhusu ujenzi wa tawi hilo la CCM Ole, alisema anatamani limazike mwishoni mwa mwaka huu ili liwezea kutumika kwa ajili ya matayarisho ya uchaguzi mkuu wa 2020.

Alisema na yeye atahakikisha anafikisha mchango wake kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa tawi hilo, ili likamilike kwa wakati.

Akisoma risala ya ujenzi wa tawi hilo, Katib wa jimbo la Ole Yakoub Khalfan, alisema hadi kufikia hatua ya ujenzi huo, shilingi milion 7.6 zimeshatumika ambapo nguvu za wanaccm wenyewe ni shilingi milion 1 pamoja na mchango wa Mwakilishi wa jimbi hilo.

Alieleza kuwa, ili kuukamilisha ujenzi huo, hadi kuweza kutumika shilingi milion 9.5 zinahitajika ambapo  anakusudia hadi mwishoni mwa mwaka huu liwe limshakamilika.

Mjumbe huyo wa Kamati kuu ya CCM taifa amemaliza ziara yake ya siku tatu kisiwani Pemba, ambapo alitembelea hospitali ya Abdulla mzee Mkoani, uwekaji wa mawe ya msingi tawi la CCM Chumbageni, Ole, Ukunjwi, skuli ya Micheweni, ujenzi wa nyumba za Polisi pamoja na skuli ya Ali Khamis camp.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.