Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar. Mhe. Vuai Mwinyi, akizinduz Kampeni ya Uvaaji wa Viatu kwa Watoto wa Vijiji vya Kijini na Mbuyu Tende Mkoa wa Kaskazini Unguja, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Zanzibar Limited Mr. Saleh Mohammed Said, uzinduzi huo umefanyika katika Viwanja vya Skuli ya Sekondari ya Kijini Matemwe Mkoa wa Kuskazini Unguja.
Best of Zanzibar yazindua
kampeni yake ya Valisha Mtoto Viatu (Pair for Every Child Campaign) katika
shule za Mbuyu Tende na Kijini wilaya Kasikazini A Unguja. Watoto wa vijiji
hivi wana tembea muda mrefu shuleni bila viatu na wengi wao hutembea zaidi ya kilomita
5 kwenye ardhi kavu ya mawe iwe masika au kiangazi.
Kutokana na hali hiyo
watoto wengi wanaweza kupata maradhi wakati wanakwenda chooni ama kukanyaga
vitu vya hatari vinavyoweza kuwadhuru.
“Best of Zanzibar
imeshafanya elimu ya afya na usafi wa mwili na mazingira, elimu hii
isingekamilika kama tusingewavisha watoto hawa viatu na ndio maana tumeanzisha
kampeni hii. Lengo letu ni kuhakikisha kila mtoto anakwenda shule na viatu kwa
ajili ya afya yao na kuboresha ufanisi wao katika masomo. Tuna hamashisha
makampuni, watu binafsi na sekta mbali mbali kuungana nasi katika kampeni hii.
Tumeanza na Kijini na Mbuyu Tende lakini shabaha yetu ni kuwavisha watoto wote
wanaokwenda shule bila viatu Zanzibar nzima.”
alisema meneja wa huduma za jamii Aminata Keita.
“Leo tuna Furaha kubwa
kuzinduliwa kwa kampeni hii katika shule yetu ya Kijini. Wazazi na walimu wa
Kijini wana furahia kuvishwa watoto wao viatu na kuonekana wamependeza na
kuhifadhika miguu yao” Mwalimu Mkuu wa Sekondari Kijini, Ulimwengu Mkadam
Uzinduzi huu uliadhimishwa
na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Vuai Mohamed akiambatana na Mkurugenzi
wa Elimu Maandalizi na Msingi Zanzibar Bi Safia Rijal, alitoa wito kwa wengine
kuunga mkono kampeni hii sio tu kwa watoto wa Kijini na Mbuyu Tende bali kwa
Zanzibar vijijini kote.
“Tunaipongeza Best of Zanzibar kwa kazi nzuri
na program zao zote kwa nia ya kuongeza ufanisi na ubora wa elimu Kijini na
Mbuyu Tende. Kwa hakika wamekuwa mfano bora wa kuigwa na taasisi nyengine
katika kuleta mabadiliko bora ya kielimu nchini.
Uzinduzi wa kampeni hiyo
uliambatana na kupewa zawadi kwa wanafunzi takriban 45 ambao wamefanya vizuri
katika Program ya masomo ya ziada ijulikanayo “After-hours Tutoring Program”
pia kutambua mwanafunzi Makame Kidawa Mwiga aliyefaulu michupuo na Vuai
Ali Haji aliyeweza kufaulu kuendelea A-Level.
Best
of Zanzibar inawakaribisha wadau wote kuungana nao katika Kampeni hii kusaidia
kuwavisha viatu watoto hawa, ili kuwafanya waweko salama kutokana na kudhurika
miguu yao na matatizo mengine ya kiafya ambayo yanaweza kuwaathiri katika
masomo yao.
Unaweza
kuungana nasi kubadilisha maisha ya watoto hawa kwa kuwasiliana kupitia
mitandao ya kijamii
No comments:
Post a Comment