Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kulizindua rasmi Jengo la Tawi la CCM Mpapa ndani ya Jimbo la Uzini.
Balozi Seif akipokea mchango wa Fedha Milioni 19,600,000/- kutoka kwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Hoh’d Raza Hassanali kwa ajili ya kuvisaidia Vikundi 97 vya Wajasiri amali wa Shehia 17 za Jimbo la Uzini.Kati kati yao ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unaguja Mh. Hassan Khatib Hassan.
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mheshimiwa Moh’d Raza Hassanali akimkabidhi Balozi Seif Printa kwa ajili ya Skuli ya Sekondari ya Uzini iliyomo ndani ya Jimbo hilo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif akimkabidhi Mwenyekiti wa CCM Mkoa Kusini Unguja Nd. Ramadhan Abdulla Ali Shilingi Milioni 19,600,000/- zilizotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Raza kwa ajili ya kugaiwa walengwa wa Vikundi vya Ushinrika ndani ya Shehia zilizomo kwenye Jimbo hilo.
Balozi Seif akizungumza na Viongozi na Wana CCM katika Mkutano wa ndani mara baada ya kulizindua Jengo la Ofisi ya CCM Tawi la Mpapa.Wa kwanza Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Kusini Unguja Ndugu Ramadhan Abdulla Ali na Kulia ya Balozi Seif ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa huo Nd. Hassan Khatib Hassan.

Baadhi ya Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wa Tawi la CCM Mpapa wakifuatilia mbambo mbali mbali yaliyojitokeza wakati wa uzinduzi wa Tawi lao.
Balozi Seif akiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Kusini Nd. Ramadhan Abdalla Shaaban kurejea nyumbani mara baada ya kuzindua Jengo Jipya la Tawi la CCM Mpapa.
Picha na – OMPR – ZNZ.
No comments:
Post a Comment