Habari za Punde

Bomba la maji kutoka Chemchem ya Mtopepo laharibika

 Kumetokezea maharibiko katika eneo la Mtopepo bomba la gravity kutoka chemchem . Maharibiko hayo yamesababisha ukosefu wa huduma ya maji katika maeneo ya Mji Mkongwe Wilaya Mjini Mkoa Mjini Magharibi Unguja.

Mamlaka ya Maji Zanzibar tayari imeshachukua hatua ikiwemo kukagua athari na kesho asubuhi mafundi wataenda kufanyakazi ili kufanikisha huduma ya maji kurejea kwa wananchi wa maeneo ya Mji Mkongwe.

Aidha, Mamlaka ya Maji Zanzibar itatoa taarifa kamili kwa wananchi juubya kilichotokea na athari zilizotokea.

Wananchi tunawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na jitihada zinachukuliwa kurekebisha maharibiko yaliyotokea.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.