Habari za Punde

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Raya Issa Msellem Azungumza na Waandishi wa Habari Kukamilika kwa Matayarisho ya Mkutano wa Baraza

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Raya Issa Msellem akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na kuaza kwa Mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi linalotarajiwa kuaza kesho 9/5/2018 na Kujadili Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kuwasilishwa kwa Maswali 279.
Kujadili Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa mwaka wa Fedha 2018/2019, .Na kuwasilishwa kwa Miswada ya Sheria itawasilishwa na kujadiliwa, Miswadi yenyewe ni 
i.Mswada wa Sheria ya Fedha (Finance Bill)    
                                          ii.Mswada  wa Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali kwa Mwaka                      2018/2019.                                                                       
Ripoti ya Mdhbiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mwaka 2015/2016.
               Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa Kazi za Mamlaka ya Kuzuiya Rushwa na Uhujumu wa                 wa Uchumi Zanzibar 2017.                                                                                           
                                                            

KATIBU wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Raya Issa Msellem akizungumza na waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na kukamilika kwa maandalizi ya Mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi linalotarajiwa kuaza keshokutwa na kujadili Bajeti ya Serikali na kuwasilishwa Maswali 279,akionesha kitabu cha kanuni za Baraza wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi mdogo wa baraza chukwani Zanzibar
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo na Katibu wa Baraza wakati akiwasilisha shughuli za Baraza linalotarajiwa kufanyika wiki hii jumatano.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.