Habari za Punde

MKAZI WA ZANZIBAR ASHINDA BIDHAA ZENYE THAMANI YA TSH.MILIONI 1 KUTOKA JUMIA

Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey kulia akimkabidhi Bi.Patricia Philipo mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 1 baada ya kuibuka mshindi. Katikati  Mchumba wa mshindi, Bw. Mwalim Juma aliyependekeza mchumba wake  ashinde zawadi ya vyombo hivyo.

MKAZI  wa visiwani Zanzibar, Bi. Patricia Philipo amejishindia vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka Jumia kupitia kampeni iliyokuwa ikiendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ katika mwezi uliopita wa Aprili.  

Mshindi huyo alipatikana kupitia kampeni iliyoendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. Wateja walitakiwa kupendekeza mtu wao wa karibu ambaye waliona anastahili nyumba yake kupendezeshwa na Jumia kwa kupatiwa ofa ya vyombo vya ndani.

Bi. Patricia Philipo aliibuka mshindi baada ya mchumba wake Bw. Mwalim Juma Kumpendekeza ashinde zawadi ya vyombo hivyo ili kumrahishia asije kusumbuka kununua tena pindi watakapofunga ndoa.

“Mimi ni mteja mzuri wa Jumia kwa sababu naitumia mara kwa mara kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali ambazo zimekuwa zikinifika mpaka ninakoishi Zanzibar. Baada ya kuliona hili shindano, niliona ni vema nimpendekeze mwenzangu ashinde. Ukizingatia tupo kwenye maandalizi ya ndoa yetu, suala la mahari pamoja na vyombo vya ndani ni gharama hivyo ushindi wake ungekuwa na mchango mkubwa kwenye shughuli yetu,” alisema Bw. Juma ambaye ni mchumba wa mshindi wa kampeni hiyo, Bi. Patricia.


“Sikuwa na wasiwasi kwamba endapo angeshinda asingeweza kupatiwa zawadi zake. Kwa sababu hapo nyuma kulikuwa na mashindano kadhaa kama vile ‘Treasure Hunt’ kipindi cha Mobile Week, wateja walikuwa wanashinda simu na kukabidhiwa bila ya ubabaishaji wowote,” alimalizia Bw. Juma.


Akielezea furaha yake mara baada ya kutangazwa mshindi Bi. Patricia Philipo amesema kuwa, “kusema ukweli hapo mwanzo sikutarajia kama ningeweza kushinda kutokana na ushindani mkali kutoka kwa mpinzani wangu. Kuna wakati nilitaka kukata tamaa kwa sababu mwenzangu alikuwa ameniacha mbali, mashabiki wake walikuwa wanamuunga mkono na kuwashirikisha wengine kwa kiasi kikubwa.”


“Lakini niliongeza bidii na kumuomba Mungu ili niweze kufanikiwa. Na kweli ilifika mahala mpinzani wangu akakata tamaa. Hapo ndipo mimi nilipoongeza bidii zaidi na kufanikiwa kuibuka mshindi,” aliongezea Bi. Patricia na kuhitimisha, “nina furaha kubwa katika kipindi hiki kwani zawadi niliyoshinda ni kubwa. Vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni moja si jambo la kawaida. Jumia wameweka alama kubwa katika maisha yangu na nawaombea waendelee kuwajali wateja wao kwa bidhaa bora, ofa lukuki pamoja na kuwa waaminifu.”


Kampeni ya ‘Big Home Makeover’ kutoka Jumia iliyodumu kwa takribani mwezi mmoja, ilikuwa na dhamira ya kuwawezesha wateja wake kununua vyombo vya ndani kwa gharama nafuu. Lakini pia ilitoa fursa ya kumzawadia mteja mmoja aliyependekezwa na mtu wake wa karibu vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni mmoja. 


“Tunampongeza mshindi wetu Bi. Patricia kwa ushindi aliojipatia lakini pia tunawasihi wateja wetu kuchangamkia bidhaa mbalimbali kwenye mtandao wetu. Kupitia mtandao unaweza kuokoa muda na gharama pamoja na usumbufu wa kufuata bidhaa. Lakini cha muhimu ni njia salama na ya uhakika, Jumia inawapatia fursa wateja wake kufanya manunuzi na kisha kulipia baada ya kuridhika na mzigo aliofikishiwa,” alisema Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey.


“Hivi sasa kupitia mtandao wetu tunaendesha kampeni ya kutoa punguzo kubwa la bei ambalo hauwezi kupata sehemu yoyote. Kwa mfano, simu zinazouzwa Jumia ni pungufu ya shilingi 50,000 tofauti na ukienda kwenye maduka moja kwa moja, vivyo hivyo kwa bidhaa nyinginezo, kila bidhaa utakayoiona basi ujue imepunguzwa kiasi hicho! Tunawasihi watanzania wasicheze mbali na jumia ili kuweza kunufaika na mambo haya mazuri,” alihitimisha Geofrey.      
 Mchumba wa mshindi, Bw. Mwalim Juma aliyependekeza mchumba wake  ashinde zawadi ya vyombo hivyo ili kumrahishia asije kusumbuka kununua tena pindi watakapofunga ndoa akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa hundi iliyofanyika Dar es Salaam jana.
 Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey.
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa mshindi huyo akikabidhiwa hundi yake.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey 
( kulia), akimkabidhi Bi.Patricia Philipo mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 1 baada ya kuibuka mshindi. Katikati  Mchumba wa mshindi, Bw. Mwalim Juma aliyependekeza mchumba wake  ashinde zawadi ya vyombo hivyo.
Click here to Reply, Reply to all or Forward

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.