Habari za Punde

Mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar.Kuaza kwa Hutuba ya Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Kuwasilisha.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akiongoza Mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar lililoaza katika Majengo la Baraza Chukwani Zanzibar.Kwa kuwakilishwa kwa Maswali na Kuchangia Hutuba za Bajeti za Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Mwaka 2018/2019.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi akiwasilisha Hutuba ya Bajeti ya Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha 2018/2019. kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuichangia. Wakati wa Mkutano wa Kumi Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar linalofanyika katika Majengo ya Baraza Chukwani Zanzibar.  
Maofisa wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakifuatilia Hutuba ya Bajeti ya Wizara yao ikisomwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, kwa Wajumbe wa Baraza. 
Wajumbe wakifuatilia hutuba ya Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakati ikiwasilishwa katika Mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar linalofanyika katika Ukumbi wa Baraza Chukwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.