Habari za Punde

Uzinduzi wa Mpango wa Uzazi Zanzibar.

Na Ramadhani  Ali /Maelezo 
Waziri wa Afya Hamad Rashidi Mohamed  amesema asilimia 30 ya vifo vitokanavyo na uzazi wakati wa kujifungua  vinaweza kuepukika iwapo huduma za uzazi wa mpango utakua unatumika vizuri.
Amesema Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa na kiwango kikubwa cha vifo vya akinamama vitokanavyo na uzazi wakati wa kujifungua na  baada ya kujifungua na vifo vya watoto wachangaga.
Waziri Hamad Rashid ameeleza hayo alipokuwa akizindua Mpango wa utekelezaji wa uzazi wa Mpango wa miaka minne Zanzibar katika Hoteli ya Ocean View Kilimani.
Alisema lengo kuu la Mpango wa uzazi wa Mpango kwa Zaanzibar  ni kupangilia uzazi kwa afya bora ya mama na mtoto , jamii na taifa kwa jumla na  sio kwa malengo mengine kama baadhi ya wananchi wanavyofikiria.
Alibainisha kwamba  ukuaji wa watu Zanzibar upo kwa kiwango cha asilimia 2.8 kwa mwaka na katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ukuwaji umefikia kiwango cha asilimia 32.8 ambacho ni kikubwa sana.
Alieleza kuwa uzazi wa mpango una faida nyingi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa jumla kiuchumi na kijamii  kama upatikanaji wa njia za uzazi wa Mpango  zinatumiwa na wananchi waliowengi.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalishughuilikia idadi ya watu (UNFPA) Jacquline Mahon alisema kuwepo mkakati  matumizi ya huduma za uzazi wa mpango Zanzibar ni  kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi  na ni chachu ya kuharakisha maendeleo .
Alisema Mpango huo utaisaidia Serikali na wadau wa maendeleo katika kufikia malengo ya kuongeza matumizi ya njia za uzazi kutoka asilimia 14 hadi kufikia asilimia 20 itaka[pofika mwaka 2022.
Jacquline alikumbusha  kuwa katika kufikia uchumi wa viwanda na kufikia malengo endelevu ya dunia matumizi ya uzazi  wa mpango ni kigenzo muhimu sana kinacho hitajika na ameahidi kuwa UNFPA itaendelea kufanyakazi na Serikali ya Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wadau mbali mbali katika kuhakikisha malengo ya mpango huo yanafakiwa.
Akiwasilisha mada ya  matumizi ya huduma ya uzazi wa mpango katika uzinduzi huo Mhadhiri wa ChuoKikuu cha Taifa Zanzibar Dkt. Issa Haji  Ziddi alisema dini ya kiislamu haijakataza kutumia njia hizo iwapo mtumiaji hazitamletea madhara.
Wakitoa mchango wao washiriki katika uzinduzi huo wakiwemo wajumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi  waliwashauri akina baba kuwaruhusu wake zao kujiunga na huduma za uzazi wa mpango kwani imeonekana baadhi yao wamekuwa kikwazo kikubwa kwa wake zao. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.