Habari za Punde

Urusi 2018: Neymar awekwa kikosi cha Brazil cha Kombe la Dunia licha ya jeraha

Chanzo cha Habari BBC.
Brazil wamemtaka mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, ambaye bado anauguza jeraha, katika kikosi cha wachezaji 23 ambao wanatarajiwa kuchezea taifa hilo katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi.
Neymar, 26, alifanyiwa upasuaji mwezi Machi na daktari wa timu ya taifa ya Brazil alisema hataweza kucheza kwa miezi mitatu.
Wachezaji wanne wanaochezea Manchester City Ederson, Danilo, Fernandinho na Gabriel Jesus ni miongoni mwa wachezaji wanaosakatia gozi Ligi ya Premia ambao wamo kwenye kikosi hicho.
Wengine ni nyota wa Liverpool Roberto Firmino na winga wa Chelsea Willian.
Beki wa kulia wa PSG Dani Alves atakosa michuano hiyo baada ya kupata jeraha la goti wiki iliyopita.
Brazil wamo Kundi E na Costa Rica, Serbia na Uswizi na watacheza mechi yao ya kwanza Jumapili 17 Juni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.