Na.Salmin Juma , Zanzibar
Waisilamu Zanzibar na duniani kwa
ujumla wametakiwa kuwa makini katika maisha yao kwa kutojiingiza katika dhulma kwani ni tendo lililoharamishwa na lisilo
takiwa kabisa kwa muisilamu yoyote yule.
Hayo yamesemwa leo na mkurugenzi wa jumuiya ya Afatah Charitable
Association Sh:Rashid Salim Mohd katika ukumbi wa S.H.A Timber hall Mombasa Zanzibar
kupitia mhadhahara uliyowakutanisha wanawake kutoka sehemu tofauti ya Zanzibar.
Akizungumza na umma uliyojitokeza katika
muhadhara huo Sh Rashid , amesema katika maisha ya leo, jambo la
kushangaza dhulma inaonenkana kama maji
ya kunywa (jambo la kawaida) na baadhi ya watu huwashangaa wengine kisa tu maisha
yao wanajiepusha na tendo hilo chafu.
‘’dhulma katika maisha ya leo imekua
ni jambo la kawaida kufanywa, watu wanaiba waziwazi, hata wanawake wanaonekana
kuiba madukani ’’ alisema sh Rashaid
Akiifafanua zaidi Dhulma amesema kitaalamu
ipo katika sehemu tatu na zote hizo zimekua ni kawaida katika maisha ya
waisilamu wa leo.
Amesema aina moja ni ile dhuluma ya mja kumdhulumu mola wake
‘’katika dhuluma hii waisilamu wengi wanajisahau mfano, kumshirikisha mungu na
kitu chengine, wapo wanaoabudu waganga wa kienyeji, kila kitu ni kwa kutizamia
, haamini kudra za mungu wake hili ni tatizo kubwa sana’’ alisema Sh Rashid
Aina ya pili ya dhuluma, amesema ni
dhuluma ya mtu kujidhulumu nafsi yake ‘’kuipelekea nafsi katika mambo ambayo
Mungu ameyakataza, wapo wasiofunga na kula mchana wa ramadhani kwa makusudi,
wapo wasio Sali na wengineo’’ alisema
Ni aina ya mwisho ya dhulma Sh Rashid
amesema ni dhuluma kubwa ambayo watu wamekua wakijiingiaza huko wengine kwa
makusudi , ni dhuluma ya kudhulumiana mtu na mtu .
Amesema , ni hali ya kuhuzunisha mno
kumuona mtu anaendesha maisha yake yote kupitia dhuluma hii, wapo
wanaowadhulumu mayatima kuendesha maisha yao, inafikia hatua mtu hali mpaka akadhulumua.
‘’dhulma mbaya sana kila mmoja ni
lazima ayatazame maisha yake la si hivyo huwezi kuepuka adhabu za Alla SW na
tufahamu kuwa yoyote anaekula mali ya haramu dua yake haikubaliwi’’ alisema
Akimalizia kuzungumza na umma huo Sheikh.Rashid amesema kuwa , matukio mabaya makubwamakubwa yanayoonekana kutokea
duniani kama vile wizi, unyang’anyi wa nguvu, na mabalaa mengine mengi yao
huchangiwa na watu kula mali za dhuluma, amesema hata watoto wengine wanazaliwa
katika misingi ya dhuluma hivyo ndio maana maisha yanakuwa magumu na ya
mitihani kila siku.
Kwa upande wao wanawake waliyoshiriki
katika muhadhara huo wamesema kuwa, kutokana na hali za kimaisha zilivyo hivi
sasa bila shaka mada iliyozungumzwa inakwenda sawa na mazingira yalivyo.
Sulha Maulid Ali amesema ,
unapozungumzia dhuluma , huwa unagusa maisha ya watu wengi hasa wanawake katika
kipengele cha dhuluma ya mja kwa mja ‘’muhadhara ni mzuri sana na napendekeza
uendelee hadi ramadhani imalizike kwani mengi yanatugusa wanawake’’alisema
Sulha.
Mwanajuma Mussa Seif kwaupande wake
amesema kuwa, awali alikua hajui mambo mengi lakini mara baada ya kuhudhuria
mhadhara huo amejifunza mengi na atakua ni mwenye kubadilika kutokana na
mawaidha hayo.
Kwa pamoja wametoa wito kwa waisilamu
nchini kujitathmini katika njia zao za kujipatia kipato kusiwe na chembe ya
dhulma kinyume na hapo maisha yatazidi kuwa magumu na mitihani.
No comments:
Post a Comment