Habari za Punde

Benki CRDB Tawi la Pemba Wafuturisha Wateja Wao.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba , Hemed Suleiman Abdalla, akisubirikupatiwa Chakula cha Futari iliondaliwa na Benk ya CRDB huko katika Wilaya ya Mkoani Pemba , wakati akijumuika na Benk hiyo kwa ajili ya kuwafutarisha Wananchi wa Wilaya hiyo.
Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa katika futari ya pamoja ilioandaliwa na Benk ya CRDB Tawi la Pemba , kwa ajili ya Wananchi wa Wilaya ya Mkaoni 
Meneja wa Benk ya CRDB Tawi la Pemba, Ahmed Abuu Bakar , akitowa maelezo machache juu ya kuwepo kwa Benk hiyo na umuhimu wa Wananchi kujiunga nayo.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla, akitowa nasaha zake kwa Waumuni wa Dini ya Kiislamu juu ya kusaidiana na kufanya mambo mema katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani , wakati akijumuika pamoja na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Wilaya ya Mkoani Pemba katika futari ilioandaliwa na Benk ya CRDB Tawi la Pemba.
(Picha na Habiba Zarali -Pemba)



Na.Habiba Zarli -Pemba.
Wananchi kisiwani Pemba wametakiwa kusaidiana katika mambo mema nayenye  kheri kwao kama Mwenyeezi Mungu (SWT), alivyoamrisha katika kitabu chake kitukufu cha Quraan.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla, alitowa nasaha hizi huko Mkoani Kisiwani humo wakati alipokuwa katika futari ya pamoja ilioandaliwa na Benk ya CRDB Tawi la Pemba kwa Wanachama wake na Wananchi kwa ujumla.

Alisema iwapo Waumini wa Dini ya Kiislamu watazingatia na kuyafuata yale ambayo Mwenyeezi Mungu , amewaambrisha na kuyawacha yale aliowakataza ni wazi kuwa watafanikiwa katika mambo yao yote ikiwa ni hapa Duniani  na kesho mbale yake.  

“Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananchi kwa ujumla niwaombeni muendelee kufanya mambo mema hata pale Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa sababu sisi Wanaadamu tumeumbwa kwa dhamira kubwa ya kumcha Mwenyeezi Mungu hivyo katika Mwezi huu ni wa kukithirisha Ibada kwani malipo yake ni makubwa ,” alisema.

Alifahamisha katika mwezi mtukufu wa Ramadhani Waumini wa Dini ya Kiislamu wanatakiwa kukithirisha ibara kwa kusoma Quraan , kuswali Swala mbali mbali zikiwemo za Faradhi na Sunna na kuswali Taraweikh na kusimama usiku kwa ajili ya kumuomba Allah SWT, na mengi mengineyo ikiwemo kuwasaidia wasiojiweza.

Alieleza kufutarisha kwa Benk ya  CRDB ni moja katika jambo muhimu sana hasa pale Mwenyeezi Mungu alipo sisitiza kuwa kuwa kumfutarisha mwenzako tone moja la maji kuna fadhila kubwa.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Kusini Pemba , aliwataka Wananchi kuitumia Benk ya CRDB kwani kuna fursa  nyingi na kusema kuwa imedhamiria kufunduwa utowaji wa huduma kwa misingi ya Kiislamu hivyo ni ni fursa kubwa ya kuitumia.

Aliwahakikishia Watendaji wa Benk hiyo kuwa Serikali itaendelea kutowa ushirikiano ili kuhakikisha wanaendelea kufanyakazi walizokusudia .

Alisema ujio wa Benk ya CRBD, Mkoani itakuwa ni chachu ya kuleta maendeleo hasa ukizingatia ndio ndio Wilaya inayochangia zaidi ya asilimia 50 katika zao la Karafuu.

Mapema Meneja wa Bank ya CRDB, Tawi la Pemba, Ahmad Abuubakar,  alisema lengo la ujio wa Benki hiyo ni kumkombowa Mwananchi na kumuinuwa Mkulima wa Karafuu .

Alifahamisha Benk hiyo itahakikisha Mkulima huyo anaondokana na Unyonge kwa kuwapatia Vifaa mbali mbali  wanavyostahiki wakati wa uvunaji wa zao la Karafuu.

Meneja huyo, alieleza kuwepo kwa Bmk nyingi sio ugomvi lakini ni sababu moja ya kuleta ushindani wa kibiashara ambao utaweza kusukuma mbele Shughuli za Kimaendeleo katika nchi.

“Wananchi karibuni katika Benk hii ili muweze kuzitumia fursa zilizopo ambazo zitatolewa kwa ajili ya manufaa yenu na Taifa kwa ujumla,” alieleza Meneja.

Kwa upande wao Wananchi waliohudhuria katika futari hiyo waliishukuru  Benk ya CRDB kwa kuona umuhimu wa kufutari pamoja na Wananchi wa Wilya ya Mkoani ambapo wameanza kuonesha mwanga kwa Wananchi w kuhusu upatikanaji wa huduma za Kibenk.

“Tunaushukuru Uongozi wa benk hii kwa kuonesha kutujali na kuamuwa kukaa nasi pamoja katika jambo hili muhimu kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani na sisi tunawaahidi tutakuwa pamoja nanyi,”walisema.

CRDB ni Benk Kongwe nchini Tanzania ambayo ina Matawi yasiopunguwa 152 ambapo kwa Afrika Mashariki inatowa huduma zake katika nchi ya Burundi .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.