Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar Maswali na Majibu.


Mwakilishi wa Jimbo la Paje Zanzibar Mhe. Jaku Hashm Ayoub, akiuliza swali kuhusiana na Matendo ya udhalilishaji yamekuwa mengi na tunatambua juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na vyombo vyake vinavyopambana na hali hiyo, Hata hivyo imeonekana kuna baadhi ya wakubwa wa Serikali wanaingilia kesi za ubakaji na kuwakingia kifua watuhumiwa. Mnamo tarehe 15/32018,Kamati ya Katiba,Sheria na Utawala ya Baraza la Wawakilishi imepata malalamiko Pemba kuna baadhi ya wakubwa Serikalini wanaingilia kazi za Jeshi la Polisi wanapowachukulia hatua watuhumiwa wa uhalifu wa udhalilishaji. 

(a) Je, Serikali inatambua viongozi wa ngazi mbalimbali ambao wametumia nafasi zao kuingilia kesi za udhalilishaji kwa kuwakingia kifua watuhumiwa wasichukuliwe hatua.

(b) Kwa vile ipo Tume ya Maadili ya Viongozi hatua gani zinapaswa kuchukuliwa zidi ya kiongozi yoyote ambaye anatukia nafasi yake ya uongozi kuingilia kazi ya Polisi wanaposhughulikia watuhumiwa wa ubakaji na makosa mengine.

(c) Kwanini Serikali haiwachukulii hatua viongozi wenye tabia hizo ambao wanaifedhehesha serikali ambayo imejufunga mkaja kupambana na vitendo vya  udhalilishaji na ubakaji kwa nguvu zote.
Naibu Waziri ya Nchi wa Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Akijibu Swali la Mwakilishi wa Jimbo la Paje Mhe. Jaku Hashim Ayoub ya vifungu (a) (b)  na (c) kama ifuatovya.Mhe Spika Serikali haina haina taarifa kwamba kuna viongozi wa ngazi mbalimbali ambao wametumia nafasi zao kuingilia kesi za udhalilishaji kwa nia ya kuwakingia kifua watuhumiwa wa makosa ya udhalilishaji.
Mhe. Spika kupitia Sheria za Nchi ikibainika kuwa kuna viongozi wa Serikali wanatumia nafasi zao kuingilia kesi za udhalilishaji kwa kuwakingia kifua watuhumiwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yoyote yule atakaye kiuka sheria ya udhalilishaji Zanzibar.
Amesema kuwa Sheria itachukuliwa kwa yoyote yule kiongozi atakayebainika na kosa hilo la kuingilia makosa ya udhalilishaji Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Konde Pemba Mhe. Omar Seif Abeid, akimuuliza Swali Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar kuhusiana na vibali vinavyotolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar vya upigaji wa Picha na uchukuaji wa habari katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar. Na kwa sababu miongoni mwa zipo za kigeni.

(a) Je, katika Kampuni hizo ambazo zimepewa vibali vya kupiga picha na uchukuaji wa filamu ni kampuni ngapi za kigeni zimepewa kibali.

(b) Je,katika Kampuni hizo zilizopewa Vibali zinapofanya kazi ya kupiga picha na kuchukua filamu. 
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Konde Pemba Mhe. Omar Seif Abeid, aliloulizwa.maswali yenye vifungu vya (a) na(b) 

Mhe Spika kampuni  za kigeni zilizopewa vibali vya uchukuaji wa picha katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Zanzibar na vitongoji vyake katika mwaka wa 2017 na 2017 ni kampuni kumi na tano (15) nazo kama ifuatavyo., 

Kampuni zenyewe ni  .1.ABT Associated Inc -Madagascar, 2.Rockhead Entertaiment -Canada,3,With Milk Films- South Africa,4,10-4 Africa - South Africa, 5.Jarowskij - Sweden, 6.World Share - South Africa, 7.Channel 1 - Spain, 8.Ard German Tv's Kenya, 9.2Traval Documentaries France, 10.World Fusion - Rwanda, 11.Baker Kent Production -South Africa, 12.Wild Aid -USA, 13.Al Jazeera Media Network - Qatar, 14.CBS News - USA na 15.Adam Bruzzone Photographer - Australia, hizi ndizo kampuni zilizopata kibali kuchukua picha sehemu mbalimbali za Zanzibar.

Mhe. Waziri Mahmoud amesema Zanzibar imenufaidika na kuitangaza Zanzibar katika Utalii kupitia uchukuaji wa picha hizo katika vyombo vya habari vya kimataifa pamoja na makampuni na mashirika makubwa ya utengenezaji wa Filam duniani kama vile Hollywood na mengine mengi duniani na pia kuingizia Mapato Serikali kupitia uchukuaji wa picha hizo.     
Mhe. Suleiman Sarahan Said Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake Pemba ameuliza swali kutotimiza Malengo Yanayopelekea Kushindwa Kwa Bajeti Kutimia, akimuuliza Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Salum Mohammed, maswali yakiwa na vifungu a,b na c amesema Serikali hufanya makisio na kupanga bajeti ili kupata mipango ya kutoa huduma kwa Wananchi na Serikali yao lakini kupanga huko hutokea baadhi ya sekta kutotimiza malengo na kufanya bajeti kushindwa kutimia na bila sababu maalum.
(a) Je, Imeshawahi kutokea baadhi ya Sekta kutotimiza malengo hayo ya Bajeti bila ya Sababu.

(b) Je,hatuoni watu kama hawa wakiendelea kushindwa kukusanya kodi ni kuturudisha nyuma kimaendeleo.                                                                                                                    

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed akijibu swali la Mwakilishili wa Jimbo la Chakechake Pemba Mhe. Suleiman Sarahan Said yenye vifungu (a) na (b) kama ifuatavyo.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina utaratibu wa kupanga mipango yake ya maendeleo ya muda mrefu na muda mfupi ili kuimarisha uchumi wake na kuimarisha upatikanaji wa huduma za msingi kwa wananchi. Aidha mipango hii hutafsiriwa kwa uandaaji wa bajeti ya Serikali ya kila mwaka ambapo sekta zote hutayarisha na kuimarisha shughuli zao katika kazi za kawaida na kazi za maendeleo. Uayarishaji wa Bajeti za kila mwaka huzingatia matarajio ya upatikanaji wa fedha za ndani kupitia makusanyo ya kodi na vyanzo vya kodi pamoja na matarajio ya fedha kutoka washirika wa maendeleo.
Hata hivyo wakati wa utekelezaji kunaweza kujitokeza sababu kadhaa zinazoweza kupeieka kutofikiwa malengo.Mfano ni kutofikiwa matarajio ya utendaji wa baadhi wa vyanzo vya mapato ,kuchelewa shughuli za ununuzi au changamoto nyengine za utekelezaji wa miradi,kutokamilika kwa wakati kwa masharti ya utoaji wa fedha ya washirika wa maendeleo na kadhalika.

Mhe. Spika sasa naomba kumjibu Mhe. Suleiman Sarahan Said kama ifuatavyo 
(a) Haijatokea kwa Sekta kutotimiza malengo ya Bajeti bila ya Sababu.    
            
 (b) Kama nilivyojibu katika swali lake (a) hakuna Sekta isiyotimiza malengo ya B  ajeti bila ya sababu.Kwa ujumla Serikali ina utaratibu wa ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji unaosaidia kuainisha sababu na changamoto za utekelezaji zinazojitokeza na kubainisha hatua za kuchukuliwa ili kurekebisha kasoro hizo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Lulu Msham Abdallah akijibu Swali la Mhe. Suleiman Sarahan Said wa Jimbo la Chakechake Pemba alilouliza Kupatiwa Stahiki Kwa Wasanii Wagonjwa na Waliofariki Zanzibar. Katika jitihada za kuwatafutia haki zao, kuendelea na maisha yao kuna watu waliofanyakazi kama kuimba au kutunga nyimbo lakini watu hao wengine wameshafika mbele ya haki au ni wagonjwa na kazi zao walizozifanya bado kuna watu wanazitumia na kupata fedha lakini hao watu waliofanya kazi hawapati malipo yoyote.

(a) Je. Wizara inalijuwa hilo.                                                                                     
(b). Je, Wizara imechukua hatua gani ili kuhakikisha watu hao wanapata haki zao.
(c).Je. Ipo Sheria ya kudai za kudai haki zao za Sanaa hapa Zanzibar.               

Naibu Waziri wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Lulu Msham Abdallah akijibu swali la Mhe. Suleiman Sarahan kama ifuatanyo lenye vifungu (a) na (b).
Mhe. Spika Wizara inalitambua hilo ndio maana Wizara kupitia Afisi ya Msajili wa Hakimiliki Zanzibar,inafanya kazi za kusimamia haki na maslahi ya wabunifu na Wasanii.Afisi hii husajili kazi za Wabunifu na Wasanii zenye sifa ya kulinwa na Sheria ya Hakimiliki. Usajili wa kazi za hakimiliki hufanywa kwa lengo la kuwatambua wamiliki halali wa kazi hizo, wakiwemo watunzi, waimbaji,waigizaji na washiriki wengine wa kazi hizo.
Aidha kuweka kumbukumbu na kutoa uthibitisho wa umiliki pale unapotokea ubishani au ukiukwaji wa haki, pia kujuwa wenye hakimiliki na ambao wanastahiki kufaidika na malipo ya matumizi ya kazi zao kibiashara.
Mhe. Spika Wizara inachukua hatua zifuatazo kuhakikisha Watu hao wanafaidika na kazi zao kupitia Hakimiliki Zanzibar.
i. Wizara kuptia Afisi ya Msajili wa Hakimiliki ina program endelevu ya kuelimisha jamii kupitia vipindi vya redio na televisheni, program za kuwafikia walengwa (Outreach Program) na mikutano ya mafunzo juu ya kuinua uelewa wa Sheria na dhana ya Hakimiliki na watumiaji wa hakimiliki kibiashara na jamii kwa jumla.

ii. Program hizi pia huelewesha juu ya umuhimu wa kusajili kazi katika Asfisi ya Msajili wa Hakimuliki Zanzibar 

iii.Wabunifu na Wasanii wote waliosajiliwa hupatiwa mirahaba kila mwaka imeazwa kulipwa tangu mwaka 2013 kwa mujibu wa matumizi yaliofanyika katika maeneo mbalimbali.Mirahaba hiyo wanapewa Watunzi, Waimbaji na watia muziki ( Music Composers) na kikundi iwapo kazi ya hakimiliki imemilikiwa na kikundi, kila mmoja kati ya watajwa hapo juu hupokea kiasi cha asilimia ishirini na tano ya kiasi chote kilichokusanywa kwa kazi husika ya hakimuliki.

iv. Vilevile ipo Sheria ya kudai haki za sanaa hapa Zanzibar;Sheria hiyo ya kudai haki za sanaa inayosimamia masuala ya ulinzi wa hakimiliki ni sheria ya Hakimiliki Namba 14 ya mwaka 2003.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.